Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chamwino Dkt. Semistatus Mashimba amesema kuwa haoni sababu ya Wilaya ya Chamwino kufanya vibaya kwenye sekta ya elimu ilihali tunawatu webye nguvu ya ushawishi bungeni na kwenye serikali.
Dkt. Mashimba ameyasema hayo hivi karibuni alipokuwa akiongea na wanafunzi wapatao 121 pamoja na Waratibu Elimu kata 36 katika gafla fupi yakuwapongeza wanafunzi bingwa waliofanya mtihani maalumu kwa lengo la kuwashindanisha wanafunzi walioshika nafasi za kwanza toka kwenye shule zao ulioandaliwa na Idara ya Elimu Msingi.
"Niwaambie ndugu zangu wilaya yetu imepata bahati kubwa sana yakuwa na watu wenye ushawishi mkubwa bungeni na serikalini, wabunge wetu wote wawili Mhe. Livingstone Lusinde(jimbo la Mvumi) na Mhe. Deo Ndejembi (jimbo la Chamwino) wanafanyakazi nzuri sana kusaidia suala la elimu katika Halmashauri yetu" Amesema Dkt. Mashimba.
Naye Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi Mwl. Zaina Kishegwe akitoa maelezo mbele ya Mkurugenzi Mtendaji amemueleza kuwa mtihani huu maalumu una lengo la kuwashindanisha wanafunzi bingwa wa kila shule waliofanya mtihani wa mock Mkoa na kushika nafasi za kwanza kwenye shule zao ilikuwaandaa vizuri kwa mtihani wao wa kuhitimu elimu ya msingi unaotarajiwa kufanyika nchi nzima mwanzoni mwa mwezi wa 9 mwaka huu.
Katika mtihani huo maalumu mwanafunzi Fransisco Chahe toka shule ya msingi Mvumi Misheni aliibuka mshindi wa kwanza miongoni mwa wanafunzi 121 waliofanya mtihani huo na kuzawadiwa jumla ya Tshs. 100,000/= pamoja na shule yao kupewa jiko la gesi na dazeni moja ya vikombe vya chai.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.