Mkuu wa wilaya ya Chamwino mhe Gift Msuya msuya amekemea vikali wafugaji wotewatakaokaidi zoezi la chanjo Wilayani Chamwino. kwakuwachukulia hatua kali dhidi ya wafugaji wote watakaokwepa zoezi la kuchanja mifugo yao wilayani hapa.
Mhe Msuya ametoa kauli hiyo hivi leo alipoongoza zoezi la utoaji chanjo kwa wanyama lililofanyika kiwilaya katika tarafa ya Mpwayungu kata ya Mpwayungu kijiji cha Mpwayungu leo tarehe 01 julai, 2021.
"Ipo tabia kwa baadh ya wafugaji hawachanji mifugo yao mwisho wa siku ikitokea magonjwa ya milipuko kwa wanyama hupelekea kufa nakuanza kuilaumu serikali kuwa haiwajali wafugaji, niwahakikishie kama serikali ya wilaya tutawashughulikia watu hao kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu", amesema Mhe Msuya.
Aidha Mhe Msuya amesema suala la chanjo ni muhimu kwa mifugo kwani husaidia kupata mifugo bora na yenye afya njema isiyokuwa na magonjwa ambayo husaidia kuongeza uchumi wa mfugaji mmoja mmoja
‘’Lazima kuwepo na ufugaji wenye tija ,tuwaelimisha wafugaji kufuga kisasa pamoja nakuwa na mifugo michache ambayo itatafutiwa malisho ,kuogesha,kuidhibiti na kuipa chanjo’’amesema Msuya.
Wakati huo huo Mhe. Msuya amebainisha kutokuwepo kwa majosho yakutosha,malambo ya kunyweshea,kutokuwepo kwa maeneo yaliyotengwa kwaajili ya kiangazi na huduma za chanjo kutolewa kwa kususua, hivyo ameagiza kila Kata kuhakikisha wanaandaa mpango mkakati kuhakikisha kila Kata inajenga josho moja na malambo ya kunyweshea mifugo.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Chama cha wafugaji Reginald Malima Lubeleje amesisitiza wafugaji kujitokeza kuchanja mifugo yao ili iwe na afya imara
Nao wafugaji waliojitokeza wameeleza umuhimu wa kuchanja mifugo yao kwani inasaidia mifugo kuwa imara hata ikipelekwa kwenye soko inauzika kiurahisi.
Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Dkt Christopher Skombe amesema kuwa Halmashauri imejipanga kuchanja mifugo ilikuwalinda na magonjwa mbalimbli ukiwemo na huu wa homa ya mapafu, tunategemea kwamba mpango wetu ni kuchanja ng’ombe zaidi ya laki mbili na mbuzi elfu sabini kwahiyo wito wangu kwa wafugaji wote wa Wilaya ya Chamwino kujitokeza kwa wingi katika zoezi hili la uchanjaji mifugo ili kuifanya Chamwino kuwa salama dhidi ya homa ya mapafu.
Naye Antony Stanslaus Mtaalamu toka Agrosteps wanaoshughulika na zoezi hilo amesema wanatoa chanjo kwa mujibu wa miongozo iliyowekwa na serikali ‘’tunaomba wananchi wa hapa wajitokeze bila kuficha mifugo yao ili iweze kupatiwa kinga’’
Mifugo inayochanjwa Wilayani Chamwino nipamoja na Ng’ombe, Kondoo na Mbuzi ambayo itasaidia kuwaepusha na magonjwa mbalimbali kama vile homa ya mapafu.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.