Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mheshimiwa Gift Isaya Msuya amewaonya watendaji wote watakaohusika na miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa wilayani Chamwino.
Mh Msuya ameyasema hayo leo Oktoba 26, 2021alipokutana na madiwani, watendaji wa kata, waratibu elimu kata, wakuu washule, wenyeviti wa serikali wa vijiji, watendaji wa vijiji na Walimu wakuu wa shule za msingi katika ukumbi wa kijiji cha Chamwino Ikulu kwa lengo la kuongea nao na kutoa maelekezo ya pamoja namna yakuendesha miradi hiyo kwa pamoja na kwakushirikiana ili kuleta tija.
"Niwaonye wakuu wa shule na walimu wakuu, fedha hizi ndugu zangu ni zamoto na mkicheza nazo nitawashughulikia, sitakubali wilaya yetu ichafuliwe na watu wachache watakaofanya ubadhirifu kwenye miradi hii" Amesisitiza Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chamwino Mheshimiwa Edson Sweti kwa upande wake amemshukuru Mkuu wa wilaya ya Chmwino kwakuona umuhimu wa kuwaita viongozi wote watakaohusika na usimamizi wa miradi hiyo ilikuwe na uelewa wa pamoja namna yakushirikiana mara miradi hiyo itakapoanza.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chamwino Dkt. Semistatus Hussein Mashimba amewasihi watendaji wote wanaohusika moja kwa moja na miradi hiyo kuanza kuainisha mapema maeneo yatakayotumika kwa ujenzi ikiwa ni pamoja na kuanza kukusanya mali ghafi zinazopatikana kwa urahisi kwenye maeneo yao kama vile mchanga, mawe na kokoto kwani hii itarahisisha kukimbizana na muda mara miradi itapoanza.
Itakumbukwa kuwa hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan aligawa fedha nchi nzima kwa ajili ya Maendeleo ya ustawi kwa Taifa na mapambano dhidi ya Uviko-19 ambapo Wilaya ya Chamwino imepokea zaidi ya Tshs. 2.6 Bilioni katika sekta ya Elimu na Afya.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.