Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Gift Isaya Msuya amefanya kikao na wadau wa mazingira Wilayani chamwino pamoja na viongozi mbalimbali ngazi ya Wilaya, Kata na vijiji wakiwemo Waheshimiwa Madiwani. Kikao kimefanyika January 10, 2023 kwenye ukumbi wa Halmashauri. Lengo la kikao hicho ni kujadili na kuweka mikakati mbalimbàli ya kutatua changamoto za mazingira zinazoikabili Halmashauri ya Wilaya ya chamwino. Katika kikao hicho Mhe. Mkuu wa Wilaya alitoa maelekezo mbalimbali yakiwemo masuala ya kupanda miti ambayo ni maelekezo ya Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira ya kupanda miti ml. 1.5 kila mwaka kwa kila Wilaya. Na miti hii inapaswa kuoteshwa na wadau mbalimbali mazingira kwa kuanzisha vitalu vyao. "Na hii huko Tabora nilikotoka tulikuwa na utaratibu kila kata ilikuwa na utaratibu wa kuanzisha kitalu mahali kwenye Taasis ya Serikali au kwenye chanzo cha maji na wanapangiwa idadi ya miche wanayotakiwa kupanda na kuistawisha". Alisema Mkuu wa Wilaya. Kazi ya mazingira ni kuwatafutia mbegu na kuwapa utaalam wa namna ya kuotesha na kuitunza miche ya mbegu iliyooteshwa ili kupata miche itakayowasaidià kupanda kwenye kata husika. Maelekezo yalitolewa Mkurugenzi ahakikishe kufikia mwezi machi, 2023 kila kata iwe imeshapanda vitalu vya miti. "Natoa wito kufikia mwezi wa tatu kila kata ianzishe kitalu cha miti, ikiwemo ya kivuli na ya matunda na itagawanywa kwa muijbu wa maelekezo yaliyotolewa. Alisema Mkuu wa Wilaya. Kila kata igawiwe idadi ya miche ya kupanda kutokana na idadi ya miti waliyopangiwa kupanda kati ya miche Ml. 1.5 iliyopangiwa Wilaya na watapita kukagua. Vivyo hivyo mgawanyo ufanyike kwa kila kata kwa miche itakayotolewa na TFS na tuhakikishe miti hiyo inatunzwa, kumwagiliwa na inakuwa. Pia maelekezo ya Mkuu wa mkoa wa Dododoma kupitia kampeni ya upandaji miti kila kaya inapaswa kupanda miche mitano, miwili ya matunda na mitatu ya kivuli na atafanya ukaguzi kila Wilaya. Aliomba wadau wa madini ya ujenzi, wakandarasi waliopewa kazi za ujenzi wa barabara maji na wapenzi wa mazingira, shulè na vituo vya afya aliwaomba washirikiane kwa pamoja maana bajeti ya Kitengo cha mazingira ni ndogo sana. Katika kikao hicho wajumbe walijadili na kuweka maadhimio mbali mbali ambayo wadau wote wa mazingira, viongozi wa kata, vijiji, vitongoji na ngazi ya Wilaya watapaswa kuyatekeleza yanayohusu mazingira hususani usafi na upandaji wa miti
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.