Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Gift Isaya Msuya amefanya kikao kazi na walimu wakuu na Maafisa Elimu Kata leo Januari 19, 2023 chenye lengo la kuweka mikakati itakayowezesha Wilaya kufanya vizuri kitaaluma kwenye elimu ya msingi.
Kikao hicho kimefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ambapo alipokuwa akifungua kikao amepongeza juhudi zilizofanyika mwaka jana kwa kuendelea kulinda nafasi waliyokuwa nayo pamoja na kuongeza ufaulu kwa asilimia 0.8.
Mkuu wa Wilaya pia ametumia kikao hicho kutoa maelekezo mbalimbali yakiwemo masuala ya uandikishaji wa wanafunzi wa awali na darasa la kwanza ambao wanaonekana kurandaranda kwenye maeneo ya biashara na kilimo wafuatiliwe na kuchukua hatua ili waende shule. Aliendelea kusema kuwa walau kufikia mwezi wa pili wafikie asilimia 100 au ikipunguwa sana iwe asikimia 90.
Vilevile aliongelea kuhusu maadili ambapo kumekuwa na masuala ya ulawiti kwa wanafunzi, walimu na wanafunzi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi kwa wanafunzi kulawitiana. Alieleza wazazi wanaamini malezi ya watoto wao yanatoka kwa walimu.
Alisisitiza pia suala la utoaji wa chakula cha mchana shuleni ambapo bado liko chini. Aidha alizungumzia suala la maelekezo ya mkoa kuhusu upandaji wa miti ambapo alwataka walimu kuwasimamia wanafunzi kila mmoja apande mti na kuusimamia hadi utakapokuwa na akimaliza shule walisishwe wanaobaki.
Vilevile alielekeza kila shule na kila kata ianzishe vitalu vya miti na miche hiyo itakapokuwa tayari igawiwe kwenye taasis za Serikali ili ipandwe na kila kaya pia itapaswa kuapanda miti mitano na kuanzia mwezi wa tatu watapita kukagua.
Suala la shule kuwa chafu, alielekeza walimu wawasimamie wanafunzi kufanya usafi.
Suala la kusaini mikataba alieleza kuwa mkataba ni sheria hivyo kwa kushindwa kutekeleza yaliyomo kwenye mkataba watachukuliwa hatua. Aliendelea kueleza kuwa mitihani ya kila mwezi ndio itakayotumika kupima matokeo( performance appraisal) watakaofanya vizuri watapongezwa na watakaofanya vibaya watapewa bendera nyekundu wakapeperushe kwenye shule zao.
Aliwaomba wawe tayari kujifunza na kufanya mabadiliko. Vilevile wawe na utayari wa kupokea maelekezo ya viongozi. Wajifunze kwa wengine waliofanikiwa hawataonekana wajinga kwa kufanya hivyo.
Mkuu wa wilaya pia aliahidi kusimamia haki za walimu na watumishi wengine kama waziri wa TAMISEMI alivyoelekeza lakini alisisitiza haki iendane na wajibu.
Katika kikao hicho wajumbe walipitia na kujadili kuhusu mpango kazi wa Mkoa kuhusu elimu ya msingi pamoja na mpango mkakati maalum wa Wilaya kwa ajili ya darasa la saba.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.