Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino imeungana na Taasis nyingine Mkoani Dodoma kuazimisha siku ya Wanawake Duniani ambayo hufanyika Machi 8 ya kila mwaka.
Kwa mkoa wa Dodoma maadhimisho haya yalifanyika kimkoa Wilaya ya Kondoa viwanja vya sabasaba na kuhudhuriwa na Taasis mbalimbali zilizoko mkoa wa Dodoma, Taasis za Serikali na zisizo za Serikali.
Katika maadhimisho hayo Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino imeweza kutoa wanafunzi watatu wa kike waliofanya vizuri kwa kupata daraja A kutoka katika shule za kata za Buigiri ambapo mwanafunzi aliyepata zawadi ni Furaha Bahati Lusulo, Mlowa Barabarani aliyepata zawadi ni Neema Gerad Maiko na Chilonwa ni Maria Julius Maning, pia mwanamke kinara Bibi Joanitha aliweza kupata zawadi.
Vilevile kikundi cha Ujirani mwema kutoka Kata ya Manchari kiliweza kupata zawadi ambazo zilikuwa zinatolewa kwa vikundi bora vya wanawake.
Aidha Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino imeshika nafasi ya tatu kwa utoaji wa mikopo kwa vikundi kwa Halmashauri zote za mkoa wa Dodoma na kushika nafasi ya pili kwa Halmashàuri zinazofuatilia marejesho ya mikopo na kurejesha vizuri kwa vikundi vya wanawake, vijana na wenyeulemavu vilivyopatiwa mikopo.
Katika maadhimisho hayo mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa na wanawake mkoa wa Dodoma yalibainishwa. Nawanawake waliaaswa kuhakikisha wanapiga hatua zaidi katika kushika nafasi za uongozi.
Suala la malezi ya watoto halikuachwa nyuma, wazazi walisisitizwa kuwalea watoto katika maadili mema ili kuwaepusha kujiingiza kwenye mambo maovu ya panya road na ushoga na ukatili wa kijinsia yanayoendelea kwenye jamii yetu.
Mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Staki Senyamule na viongozi mbalimbali wa Serikali walihudhuria akiwepo Waziri wa uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Ashantu Kijaji.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.