Timu ya ukaguzi wa miradi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma wakiongozana na wataalam kutoka Halmashauri leo tarehe 29 Julai, 2025 wametembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino iliyo katika mwaka wa fedha uliotangulia wa 2024-2025
Miradi hiyo iliyotembelewa ni pamoja na;
1. Ujenzi wa bweni moja katika shule ya Sekondari Chamwino
2. Ujenzi wa jengo la mionzi Kituo cha Afya Chamwino
3. Ujenzi wa machinjio ya kisasa Chamwino (eneo la mnadani)
4. Ujenzi wa jengo moja lenye nyumba mbili (2 in 1) za walimu katika shule ya Sekondari Mwl. Nyerere.
5. Ujenzi wa majengo ya shule mpya ya mkondo mmoja katika Shule ya Msingi Majeleko.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.