Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino imetoa vyeti vya pongezi kwa NGO's zinazofanya kazi wilayani humo ikiwa na lengo la kutambua mchango unaotolewa na NGO's hizo.
Vyeti hivyo vimetolewa leo kwenye kikao cha tathimini ya utendaji kazi wa mashirika hayo Mei 12, 2023 kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
Jumla ya NGO's15 zilikabidhiwa vyeti kwa vigezo mbalimbali kulingana na huduma wanazozitoa kwa jamii ya Chamwino.
NGO's ni pamoja na Katuka paralegal, Tayoa, Black Maendeleo Tanzania,EGPAF, Water Mission, Development services coordination, Innovation of Africa, Sustainable Agriculture Tanzania, SAT uwezeshaji wanawake, Children in cross fire, Restless Development, Safe Island for women, Compaign for women and children Tanzania, Doctors with Africa(KUAMM), The lead Foundation na Lay Volunteer International Association.
Mgeni Rasmi kwenye kikao hicho alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Gift Isaya Msuya ambaye aliwakilishwa na Katibu Tawala wa Wilaya Bi Neema Nyalega.
Katibu tawala amezisisitiza NGO's kuwasilisha taarifa zao za kila robo mwaka pamoja na taarifa za bajeti zao kwani zinasaidia Halmashauri kuweza kuweka mango mzuri wa kibajeti katika kutoa huduma kwa wananchi. " Nasisitiza kwa kila taasis isiyo ya Kiserikali kuhakikisha inawasilisha bajeti yake Halmashauri na jambo hili si la mzaha. Taasisi itakayoshindwa kuwasilisha bajeti hatua zitachukuliwa dhidi yake." Alisema.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.