Katika maadhimisho ya Kilele cha siku ya wakulima ( Nanenane) kanda ya Kati Agosti 08, 2023 inayojumuisha mikoa ya Dodoma na Singida ambayo yamefanyika kwenye viwanja vya maonesho ya nanenane eneo la Nzuguni Dodoma, Halmashauri ya Chamwino imefanikiwa kuchukua ushindi kwenye nafasi mbalimbali.
Nafasi ambazo Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino imefanikiwa kuzichukua mojawapo ni katika kigezo cha uwanjani( vipando) ambapo imeshika nafasi ya tatu na kuweza kukabidhiwa cheti.
Nafasi nyingine ni kwa kigezo cha mkulina bora anayetegemea mvua ambapo mkulima Aloyce Kinyonga kutoka Chamwino ameshika nafasi ya pili. Aloyce kinyonga amezawadiwa Tshs 1,125,000/= pamoja na cheti.
Katika kigezo cha mkulima bora wa umwagiliaji mkulima David Mwaka kutoka Chamwino ameshika nafasi ya kwanza na kuzawadiwa Tshs 1,500,000/= pamoja na cheti.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziŕi Mkuu Ajira na watu wenye ulemavu Mhe. Patrobas Paschal Katambi.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.