Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Dkt. Hussein Mohammed Omar ametembelea shamba la Jenga Kesho Iliyobora (BBT)Mlazo-Ndogowe, Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Novemba 30 na kukabidhi ekari 2000 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino na Serikali ya vijiji vya Mlazo na Ndogowe.
Katika ziara hiyo ya kutembelea shamba la mradi wa Jenga Kesho Iliyobora (BBT) Mlazo-Ndogowe, Dkt. omar aliambatana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Mhe. Edson Sweti, Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Ndg. Tito .P Mganwa pamoja na watumishi kutoka Wizara ya Kilimo na Halmashauri.
Dkt. Omar amesema ekari hizo 2000 za shamba la BBT Mlazo-Ndogowe sasa zitaaenda kunufaisha wananchi wa vijiji vya Mlazo na Ndogowe kwa kuanza uzalishaji ambao ekari 500 tayari zimesafishwa kwa ajili ya kuanza uzalishaji huo.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Ndg. Tito .P Mganwa amesema Halmashauri itaendelea kutoa ushirikiano kwa Wizara ya Kilimo ili miradi iliyochini ya programu ya Jenga Kesho Iliyobora (BBT) iliyopo Chamwino (Chinangali na Mlazo-Ndogowe) inakuza uchumi wa vijana.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.