Kikao cha tathimi ya utekelezaji wa mkataba wa lishe ngazi ya kata kwa robo ya tatu Januari Machi, 2024 kimefanyika leo Mei 2, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
Kikao kimeongozwa na mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya Ndg: Japhari Kikoti ambaye ni Afisa Tarafa wa tarafa ya Chilonwa.
Katika kikao hicho wajumbe wamefanya tatimini ya kadi alama na mafanikio yaliyopatikana ni kwa Halmashauri ni kuqa imetekeleza viashiria vya mkataba wa lishe ngazi ya Kata kwa kupataalama ya kijani kwa viashiria 7 kati ya 8 sawa na asilimia 87.5%
Vilevile kumekuwa na ongezeko la watoto wanaokula chakula shuleni angalau mlo mmoja kutoka 66.08% kwa mwezi Disemba hadi kufikia 69.04 kwa mwezi Machi 2024.
Ilielezwa pia vijiji vyote 107 vimefanya maadhimisho ya siku ya Afya na Lishe ya kijiji ( SALIKI) mara moja kwa robo ya Januari hadi Machi.
Aidha Halmashauri imejiwekea mikakati mbalimbali ili kuhakikisha inafanya vizuri zaidi kwenye maeneo yenye changamoto.
Wajumbe pia wamempongeza Mkurugenzi Mtendaji kwa kutoa fedha kuwezesha masuala ya lishe pamoja na wadau wote wanaoshirikiana na Halmashauri.
Pia Kata ya Msanga imepongezwa kwa kubuni mbinu ya kuaandaa bonanza la michezo siku,ya Afya na Lishe ya Kijiji jambo ambalo limeongeza hamasa ya wanaume kushiriki kwa wingi k8nyume na ilivyokuwa awali ambapo walishiriki wachache.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.