Wilaya ya chamwino imefanya tamasha la sanaa, michezo na utamaduni( ngoma za asili), mapishi na maonesho ya vyakula vya asili kwa ajili ya lishe bora ikiwa na lengo la kuenzi miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao kilele chake kitakuwa Aprili 26, 2024.
Tamasha limefanyika Kata ya Handali leo Aprili 23. 2024 na mgeni rasmi alikuwa ni Mhe. Janeth Mayanja, Mkuu ya wilaya ya Chamwino.
Akizungumza katika tamasha hilo Mkuu wa wilaya amewapongeza Halmashauri kwa kuaandaa tamasha hilo pamoja na vikundi mbàlimbàli vya ngoma, wanamichezo wote pamoja na walioandaa mapishi ya asili na wananchi wote kwa ujumla wake.
Amewasisitiza wananchi kuhakikisha wanakula mlo kamili na si kula kwa ajili ya kujaza tumbo peke yake. Ameeleza kuwa makuzi ya mtoto yanaanza pindi anapotungwa mimba hadi siku elfu moja na hivyo kuanzia hapo mama mjamzito anapaswa kula mlo kamili yaani webye makundi yote ya xhakula sambamba na kumlisha mtoto na kufanya hivyo mtoto atazaliwa na kukua na afya njema na kuwa na akili.
Aidha Mhe. Mayanja amewaasa kuuenzi Muungano kwani miaka 60 uliyofikia ni mingi na hivyo ni suala la kujivunia. Ameeleza kuwa zipo nchi nyingi zilizojaribu kuungana lakimi hawakudumu.
Vikevike mkuu wa wilaya ametumia nafasi hiyo kusikiliza kero mbalimbali za wananchi waHandali.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.