Halmashauri ya wilaya ya Chamwino imeelezea mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan.
Mafanikio hayo yametolewa leo Aprili 4, 2024 na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Ndg: Tito Philimon Mganwa kwenye kongamano la miaka mitatu ya ya dhahabu ya Samia lililoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Janeth Mayanja lililolenga kuwafikishia wananchi mazuri yaliyofanywa na Serikali kupitia Taasisi zake zilizopo Chamwino.
Kongamano limefanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino na mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Janeth Mayanja.
Akizungumza katika kongamano hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya amesema kwa kipindi cha miaka mitatu ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Halmashauri imepokea kiasi cha Tshs. 75,620,38029 sawa na 53.6% ya miradi yote iliyokuwa ikiletwa katika Wilaya ya Chamwino kupita Taasis zote za Wilaya.
Ilielezwa kuwa Shilingi bilioni 13,0893,400 kwa ajili ya kutekeleza kwa sekta ya elimu msingi na sekondari
" Mtakuwa mashahidi tulipata shilingi bl. 3 kwa ajili ya shule ya sekondari ya wasichana na inaendelea iko hatua za mwisho. Tumepata jumla ya shilingi milionil. 811 kwa ajili ya mradi wa BOOST, lakini pia tulipata bilioni 2,498,000,000/_ kwa ajili ya ujenzi wa shule za sekondari mpya za Zajilwa, Nyerere, Ndogiwe na Ndejembi" Alisema Mkurugenzi Mtendaji.
"Lakini vilevile tumepata fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 64 kwa ajili ya maeneo magumu ili kuhakikisha kwamba hakuna hata mtu mmoja anayeachwa nyuma katika elimu na hii imekuwa na thamani ya shilingi bilioni. 1,280,000,000/=, vilevile tulipata mradi wa UVIKO wenye thamani ya shilingi bl. 1 ml. 280 na vilevile tulipata fedha jumla ya shilingi bl.1,880,000,000/= kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 82 ya sekondari. " alisema Mkurugenzi Mtendaji.
Mkrugenzi Mtendaji aliendelea kueleza kuwa walipata bl. 1,083,000,000/= kwa ajili ya mradi wa Boost. Pia 390,000,000/= kwa ajili ya mradi wa SEQUIP lakini tulipata fedha nyingine 385,000,000/= kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu na ujenzi wa miundombinu mingine mabweni na vyoo.tulipata jumla ya shilingi bl. 1na ml. 26.
Aliendelea kueleza kuwa fedha hizi ambazo wamezipata zimepelekea kupunguza idadi ya wanafunzi wa darasa la nne wasiojua KKK yaani kujua kusoma, kuandika na kuhesabu kutoka idadi ya wanafunzi 302 kwa mwaka 2021hadi wanafunzi 29 tu kwa mwaka 2023.
"kumekuwa na ongezeko la ufaulu kwa wanafunzi wa darasa la saba kutoka 76.1% kwa mwaka 2021 hadi 89.6 na hivi tunaahidi kwamba muda unavyozidi kwenda kutokana na miundombinu tuliopata na uboreshaji wa mazingira na vitendea kazi tunatarajia kufika 100% ." Alisema Mkurugenzi Mtendaji.
Aidha ameeleza kuwa kutokana kupata fedha hizo ufaulu wa kidato cha nne umepanda mwaka kwa mwaka na kumekuwa na ongezeko la ufaulu kutoka daraja la kwanza hadi la nne kwa kidato cha sita kutoka 39.4 2021 hadi 100% kwa mwaka 2023 na haya ni mafanikio makubwa.
Kwa upande wa Idara ya Afya kwa miaka mitatu tumepata miradi mbalimbali yenye thamani ya shilingi bl 7,400,085,429 ambayo imejenga hospitali ya wilaya, ujenzi wa vituo 5 vya Afya vya Itiso, dabalo, Manda, Haneti na Msamalo vyenye thamani ya shilingi bl. 2,646,000,000/=
Halmashauri ilipata pia Ml. 782 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati 16, bl. 2.15 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba. Milioni.500 kwa ajili ya ujenzi wa mtambo wa usindikaji wa oksijeni hospitali ya Uhuru.
Ilielezwa kuwa fedha hizi zimepelekea uboreshwaji wa huduma za afya kwa wananchi. Kutokana na fedha hizi kumekuwa na ongezeko la vituo vya Afya kutoka 5 hadi 9, iadi ya zahanati toka 65 hadi75 katika kipindi cha miaka 3. Kumekuwa na ongezeko la huduma za mama na mtoto toka 12 hadi 82, kumekuwa na ongezeko la huduma za kulaza wagonjwa toka vituo 6 hadi vituo 9, kuongezeka kwa huduma za dharura za upasuaji toka vituo 3 hadi vituo 7, vituo vinavyotoa huduma za mionzi vimeongezeka kutoka kituo kimoja hadi vituo 6 na kuna kituo kingine kinajengwa hapa chamwino na kitakapokamilika kutakuwa na vituo 7.
Vituo vinavyotoa huduma za meno vimeongezeka kutoka kituo kimoja hadi vituo 3,kuongezeka kwa magari ya wagonjwa kutoka 5 hadi 8, kuongezeka kwa bajeti ya manunuzi ya dawa kutoka ml. 359, 623,000/= hadi ml. 710,413,124 ambazo zote hizi ni ruzuku Toka Serikali kuu. 163,900,000/= hadi kufikia 335,000,000/= kwa fedha za mfuko wa afya wa pamoja.
Kumekuwa na kuongezeka kwa watumishi kutoka watumishi 413 mpaka watumishi 508
"Tunaishukuru Serikali ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutuwezesha kutoa huduma katika eneo hili la Afya." Alisema Mganwa.
Kwa upande wa kilimo alieleza kuwa Halmashauri inanufaika na mradi mkubwa wa mashamba ya pamoja ( block farming) ambapo bl.52,322,823,000/= ambazo zibasimamiwa na Wizara ya Kilimo lakini zinafanyika katika Halmashauri na wanufaika wakubwa ni sisi na maendeleo makubwa yataletwa hapa na mradi huu.
Vijiji 13 vilivyojengewa majosho vimeongeza ufugaji wenye tija na kupunguza magonjwa kwa mifugo, wakulima 17612 wamesajiliwa kwenye mfumo wa mbolea za ruzuku. Wakulima 218 wamenunua tani 56.7 ya mbolea ya ruzuku ambayo inagharama nafuu. Vilevile kinajengwa kiwanda cha kusindika zabibu kwenye shamba la Chinangali ambacho kitaondoa kero ya soko la zabibu kwa wakulima wa Wilaya ya Chamwino na mkoa wa Dodoma kwa ujumla.
Kumekuwa na kufunguka kwa fursa za kiuchumi kwa wananchi wa Vijiji vya Mlazo, Ndogowe kwa kufikishiwa huduma ya umeme, ujenzi wa zahanati mpya ya Mlazo, uhakika wa huduma ya maji kwa visima 10 na maboresho makubwa ya barabara katika maeneo hayo.
Aidha Halmashauri imepata fedha za ujenzi wa jengo la Utawala kwa ajili ya kuboresha mazingira kiasi cha shilingi 1,900,000,000/= lenye uwezo wa kuhudumia watumishi 165 na kumbi 3 za mikutano na wigo kwa ajili ya usalama na eneo la kuhifadhi magari 75 kwa wakati mmoja.
Aidha Mkuu wa wilaya ya chamwino amezipongeza taasis zote za Serikali kwa maono , kwa uzalendo na kazi nzuri wanayoifanya na kwa namna wanavyojua dhana ya uwajibikaji na kwa hakika malengo ya kongamano yameweza kutimia. Ameona kuwa anatimu imara na hivyo mambo yatajuwa mazuri kwa kuwa anawasaidizi wanaoelewa kwa nini wapo kwenye nafasi hizo.
"Ninyi ni mashahidi yaliyofanyika Chamwino siyo ya Kufikirikani mambo yanayoonekana kwa macho. Wakuu wa taasis wamesema hapa kwa kipindi cha miaka 3 wameweza kupokea fedha takribani shilingi Bilioni 141. Tunamshukuru sana Mhe. Rais. Wilaya ziko nyingi kwa kuipendelea Chamwino kwa Miradi ya kimkakati." Alisema Mhe. Mayanja.
" lakini kwenye kila kijiji usipokuta kuna mradi wa umeme basi kuna mradi wa barabara, usipokuta barabara basi kuna mradi wa ujenzi wa nyumba ya mwalimu, kuna mradi wa ujenzi wa shule, kuna mradi wa matundu ya vyoo, ki ukweli hakuna kijiji ambacho Mhe. Rais amekiacha. Nawaomba wananchi wa Chamwino muendelee kumuombea Mhe Rais afya njema na maono ya kuendelea kuwasiaidia Watanzania hasa wananchi wa Chamwino." Alisema Mhe. Mayanja.
Mkuu wa wilaya ameomba wadau waendelee kuwekeza chamwino kwani inamiundombinu yote inayohitajika ikiwemo umeme, barabara na Ardhi na ukiangalia kwa mipango ya Mhe. Rais baada ya miaka 5 itakuwa imepiga hatua kubwa kimaendeleo,
Vile vile Mhe. Mayanja amewaomba wanachi kutunza miradi iliyopelekwa kwenye maeneo yao na hiyo itakuwa namna nzuri ya kuonyesha wanaunga mkono juhudi za Mhe. Rais na kila mmoja awe mlinzi kwa mwenize ili miradi hiyo iendelee kutoa huduma
Mhe. Mayanja pia amewashukuru mafundi mchundo kwa kutoa tuzo kwa Mhe. Rais na yeye kama mwakilishi wa Mhe. Rais amekiri kuipokea na kuifikisha kwa Mhe. Rais.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.