Leo Januari 12, 2024 ikiwa ni siku ya Maadhimisho ya Miaka sitini (60) ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Timu ya Itifaki wilaya ya Chamwino (Protocol service Team) PST Kwa kushirikiana na Taasisi ya PTO (Tanzania Patriotic organisation) wamezindua kampeni maalumu waliyoipa jina la" Nirudishe shuleni" ya kuwapatia mahitaji na vifaa vya shule wanafunzi wenye uhitaji mashuleni ili waweze kutimiza ndoto zao za kielimu.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa PST ndugu Hussein Hussein wakati akizingumza katika zoezi Hilo lililofanyika katika shule ya Msingi Buigiri wasioona (Buigiri blind school) iliyopo kata ya Buigiri wilaya ya Chamwino ambapo wameanza kwa kugawa sare za shule kwa wanafunzi 100 wa shule hiyo.
"Kwakuwa PST ni Taasisi inayoaminika katika kusimamia shughuli mbalimbali za kiitifaki za Serikali na kupitia wazo la Mkuu Wa wilaya ya Chamwino ndugu yetu GIFT MSUYA tumekuja na kampeni hii inayolenga kuwashika mkono wanafunzi wenye uhitaji na Leo Kwa umuhimu mkubwa tumeona tuanzie katika shule hii ya Buigiri kwakuwa ni nyumbani, huu ni mwanzo tu lakini tunatarajia kuzifikia shule 84 , pia niwaahidi wanafamilia ya Buigiri wasioona tutaendelea kuja zaidi ili kutoa vifaa mbalimbali vya shule kadri vitakavyohitajika." Alisema Hussein.
Kwa upande wake Mgeni Rasmi ambaye pia ni Mheshimiwa Diwani Wa kata ya Buigiri Kenneth Yindi amewapongeza PST na PTO Kwa kutambua umuhimu Wa kufanya zoezi Hilo la kizalendo kwa kusherehekea Maadhimisho ya Mapinduzi, akieleza kuwa kila mtanzania anapaswa kuwa mzalendo katika nafasi yake ili kuhakikisha ustawi wake na Taifa kwa ujumla. Pia Ametoa Wito Kwa Wananchi kusaidiana, kupendana ,kuthaminiana na kutoa taarifa za uharibifu Wa Mali za umma ama wizi unaotokea kwenye maeneo yetu katika Mamlaka husika Kama sehemu ya uzalendo.
Naye Katibu Tawala wilaya ya Chamwino Neema Nyarege ambaye pia amemwakilisha Mkuu Wa wilaya Mheshimiwa Gift Msuya katika hafla hiyo, ametumia fursa hiyo kueleza kuwa lengo la Mheshimiwa Msuya kuwashauri PST Kuja na kampeni hiyo ni jema , hivyo ofisi ya Mkuu wa wilaya iko tayari kuwaunga Mkono wakati wote ili waweze kutimiza Adhma ya kuwarudisha watoto shule Kama kampeni Yao inavyojieleza. Pia amesema mlango uko wazi Kwa Taasisi yeyote inayohitaji kufanya shughuli za kijamii na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ipo tayari kushirikiana nao.
Tukio Hilo ambalo awali limetanguliwa na zoezi la upandaji Miti katika viunga vya shule hiyo, limehudhuriwa na katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Chamwino, viongozi wa CCM kata ya Buigiri, viongozi wa Serikali kata ya Buigiri, kaimu Afisa Elimu msingi Wilaya, Katibu wa Mbunge jimbo la Chamwino, wanafunzi wa shule ya sekondari Chamwino na jumuiya ya shule ya Msingi Buigiri wasioonana.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.