Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino imeadhimisha Siku ya wanawake Duniani kwa kupanda miti ya matunda kwenye eneo la makazi ya wenye ulemavu wa macho ( Matembe bora) lililopo kata ya Buigiri Machi 04, 2024.
Makazi hayo ya wasioona yana jumla ya kaya 13 ambapo kila kaya imepatiwa miche 8 ya matunda mchanganyiko ya mapera, maembe, michungwa, malimao na mapapai.
Miti hii ya matunda imetolewa na wadau wa maendeleo kutoka shirika la Save The Children ambao pia wameahidi kutoa mbuzi wa maziwa kwa vikundi vya wakazi hao vitakavyoundwa.
Katika hotuba yake mgeni rasmi ambaye ni Katibu Tawala wa Wilaya Bi. Neema Nyalege ameahidi kushughulikia changamoto walizoziwasilisha wakazi hao ikiwemo suala la gharama za kuingiza umeme kwenye makazi yao ambapo ameahidi ofisi yake kuzilipa zote.
Mada mbalimbali kuhusu ukatili wa kijinsia, kilimo bora, lishe, mazingira, umuhimu wa kukata bima ya Afya ya jamii (CHF) iliyoboreshwa viliwasilishwa na wataalam kutoka Halmashauri kwa lengo la kujengea uelewa wakazi hao wa Matembe bora.
Shirika lisilo la Kiserikali la Para legal linalofanya kazi Wilayani Chamwino walitoa zawadi mfuko mmoja wa sabuni ya unga ambazo ziligawiwa kwa wakazi hao.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.