Wajumbe wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino wamepewa elimu kuhusu ugonjwa wa homa ya ini ( hepatitis B) ambao kwa sasa umekuwa maabukizi yake yamekuwa yakiongezeka kwenye jamii.
" imeonekana kuna ongezeko kubwa la tatizo la homa ya ini kati ya asilimia nne hadi tano kwa wale wanaokwenda kuchangia damu wamekuwa wakikutwa na maabukizi ya homa ya ini. Homa ya ini zipo za aina mbalimbali kuna A, B, C na D mpaka E." Alisema mganga Mkuu.
Elimu hiyo imetolewa na Mganga Mkuu wa wa Wilaya ya Chamwino Dr. Eusebius Kessy leo Agosti 22, 2023 kwenye kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya nne kilichofanyika kwenye ukumbwa mikutano wa Halmashauri hio.
Dr. Kessy amesema ugonjwa huu njia zake za maambukizi zinaendana na zile za maambukizi ya VVU ambapo kupitia majimaji yoyote yanayotoka kwenye mwili wa mtu mwenye maabukizi, mtu anaweza kuambukizwa ugonjwa huu.
" Homa ya ini inaenezwa kwa staili ileile inayoaeneza virus vya Ukimwi (VVU) kwa maana kupitia kujamiiana, kupitia kwa wanaokwenda saloon, lakini pia homa ya ini inaweza kuambukizwa kwa majimaji yoyote yanayotoka mwilini mwa mgonjwa wa homa ya ini." Alisema Dr. Kessy
" Kwa hio ni ugonjwa ambao unaenea kwa kasi sana na Wizara ya Afya inaendelea kutoa elimu kuhusiana na homa ya ini. Homa ya ini ikimpata mgonjwa dalili zae ni kama za malaria, mwili kuchoka viungo lakini pia inaweza kusababisha macho kuwa ya njano na mara nyingi ikitokea dalili hizi huwa zinaisha zenyewe na baadae,kinachojitokeza ni mgonjwa kupata tatizo linalopelekea kuwa na manjano lakini pia inaweza kusababisha kansa ya ini." Alisema Dr. Kessy.
Kwamtu ambaye amepatikana na ugonjwa huu atalazimika kutumia dawa kwa muda mrefu na gharama yake ni kubwa.
Amesitiza kuchukua hatua mapema ya kwenda kupata chanjo ambayo inatolewa kwenye hospitali ya Wilaya ambayo ipo Mlowa barabarani, kituo cha Afya Chamwino na hospitali ya Uhuru.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.