Maneno hayo yamesemwa na Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Chamwino Bi. Asha Shame Vuai leo tarehe 04.07.2019 alipotembelea kijiji cha Mpwayungu Wilayani Chamwino kwa lengo la kuhamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii CHF iliyoboreshwa.
Amesema kuwa Mkurugenzi Mtedaji wa Halmashauri anatenga fedha kila mwaka kwa ajili ya mikopo kwa Vijana, Wanawake na Walemavu na kutoa wito kwa wananchi wa Chamwino kuunda vikundi na kuvisajili ili wakopeshwe.
Akiwa kijijini Mpwayungu Bi. Asha ametembelea na kukipongeza kikundi cha MGANGALENGA kilichoanzisha mradi wa Machinjio na Choo cha Kulipia kwa juhudi zao na kuwaeleza kuwa Halmashauri itawaunga mkono.
Aidha Afisa Maendeleo ya Jamii amewataka wananchi kujiunga na mfuko huo ili waweze kupata matibabu ya gharama nafuu kwa kipindi cha mwaka mzima.
Mwakilishi wa Mratibu wa CHF Wilaya Abdallah Missenye amewaeleza wakazi wa Mpwayungu kuwa kiasi cha shilingi 30,000 kitawawezesha wanakaya sita kutibiwa kwenye ngazi za zahanati, kituo cha afya, hospitali ya wilaya na hospitali ya rufaa mkoani Dodoma, Morogoro, Shinyanga na Manyara.
Bw. Missenye aliongeza kuwa serikali ipo katika mchakato wa kuhakikisha mwanachama wa CHF anatibiwa kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za afya nchini kote.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.