Na Brian Machange- Babati Manyara
Timu ya michezo ya Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino yashindwa kung’aa katika bonanza la watumishi liliandaliwa kwa ushirikiano wa wadau wa michezo wa Halmashauri ya Mji Babati na Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino.
Katika Bonanza hilo lilifanyika mapema leo tarehe 28 Novemba 2020, wanamichezo wa Timu ya Mji Babati wameibuka kidedea katika michezo yote iliyofanyika katika viwanja vya Kwaraa mjini Babati Mkoani Manyara, ambapo katika mchezo wa kwanza wa mpira wa miguu timu ya Babati TC iliibuka kidedea dhidi ya timu ya Chamwino DC kwa magoli 3-1.
Netball kwa wanawake walishindwa kufua dafu mbele ya wapinzani wao timu ya Babati TC kwa kufungwa magoli 13-4
Kwa upande wa mchezo wa kuvuta Kamba Babati TC iliibuka tena kidedea kwa pande zote mbili yaani wanawake na wanaume kwa kuzishinda timu za wanawake na wanaume wa Chamwino DC iliionekana kuelemewa vibaya licha ya kuonekana watu waliokuwa na misuli yakutosha kuzikabili timu za wanawake na wanaume wa Babati TC.
Hata hivyo Chamwino DC iliibuka kidedea wa mchezo wa kukimbiza kuku kwa upande wa wanaume na kufanya angalau Chamwino kutoondoka mikono mitupu uwanjani.
Awali akifungua Bonanza hilo Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Jacob Twange amesema kuwa lengo la kufanya bonanza hili ni kudumisha urafiki baina ya watumishi wa Halmashauri ya Babati Mji na Halmashauri ya Chamwino hivyo amewataka washiriki wote wa michezo kuzingatia kanuni na sheria za michezo husika, kwani michezo ni burudani na sio uadui hivyo wawe tayari kwa matokeo yoyote.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.