Wajumbe wa Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino wametoa pongezi kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Wahe. Madiwani, Mkurugenzi Mtendaji, Mweka Hazina na Menejimenti ya Halmashauri kwa kukusanya mapato ya ndani na kuvuka lengo kwa 126% na kuongoza kwa Halmashauri za Mkoa wa Dodoma kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022.
Pongezi hizo zimetolewa leo, Septemba 07, 2022 kwenye kikao Maalum cha Baraza la mwaka kilichofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri.
Sambamba na pongezi hizo wajumbe wameshauri mambo mbalimbali yatakayosaidia Halmashauri kuendelea kufanya vizuri kwenye kukusanya mapato.
Kati ya mambo yaliyoshauriwa ni suala la watendaji wa vijiji kutoa ushirikiano kwenye ukusanyaji wa mapato. Ilishauriwa Mkurugenzi Mtendaji awape malengo ya kukusanya kwa kila kijiji.
Pia Kudhibiti utoroshaji wa mapato kwenye mageti, wakusanyaji mapato wa magetini wabadlishwe mara kwa mara, wasikae eneo moja kwa muda mrefu
Ilishauriwa pia kudhibiti utoroshaji wa mifugo minadani yajengwe maboma walau ya muda ya kwa ajili ya mifugo ambayo haijauzwa na ambayo imeuzwa kwa minada ambayo haina maboma hayo.
Vilevile ilishauriwafedha zilizokusanywa ziwasilishwe na kupelekwa benki mapema kuepuka fedha kutumika kinyume na utaratibu.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.