Na Brian Machange - Buigiri, Chamwino
Waziri wa Maji Mheshimiwa Juma Aweso (Mb) amesema hataongeza muda wa siku 60 uliotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Maji kukakamilisha mradi wa ujenzi wa tangi la maji Buigiri Wilayani Chamwino.
Mheshimiwa Waziri ameyasema hayo leo tarehe 21 Januari, 2021 kwenye ziara yakukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa tangi la maji lenye ujazo wa zaidi ya Lita 2,500,000/= ambapo litarahisisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wakazi wa Kata ya Buigiri, Chamwino pamoja na wakazi wa maeneo ya IKulu.
Mh. Aweso amewataka wajenzi wa mradi huo ambao ni SUMA JKT kufanyakazi usiku na mchana ilikukamilisha mradi huo muhimu kwa wananchi wa Wilaya ya Chamwino.
‘Sisi tunataka hili tangi kukamilika kwa wakati, na kukamilika kwa wakati ni lazima mfanyekazi usiku na mchana ili muweze kukamilisha mradi huu kwa siku zilezile 60 alizotoa Naibu Katibu Mkuu ndizo tutakazozisimamia’ Amesema Aweso.
Naye mjumbe wa Bodi ya DUWASA Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma Mh. Prof. David Mwamfupe amemuahakikishia Waziri wa Maji kuwa maagizo yote aliyoyatoa hayanakukwepa hivyo watakuwa kiungo kati yao katika kutekeleza mradi huo, kwani azima yakuhamia Dodoma sio tu kuwa na majengo makubwa lakini ni pamoja na kuimarisha huduma za maji.
Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Bi. Vumilia Nyamoga amemshukuru Waziri wa Maji kwakutembelea mradi huo na kumhakikishia kuwa watampa ushirikiano wa kutosha ikiwa ni pamoja na kuwa walinzi wa kwanza wa mradi huo mkubwa wa maji.
Akitoa shukrani kwa Waziri wa Maji, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chamwino Mh. Keneth Yindi ametoa shukrani za dhati kwa Waziri wa Maji kwa kupata mradi huu mkubwa wa maji kwani Chamwino kwa sasa inapokea wageni wengi ikizingatia kuwa makazi rasmi ya Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Mgufuli yapo hapa hivyo kufanya kuongezeka kwa mahitaji ya Maji.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.