Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Chamwino Ndg. David Mwamalasi Amefungua Mashindano ya UMISETA ngazi ya Wilaya Katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Chamwino. Aidha Mashindano hayo yenye Kauli mbiu ya "MICHEZO, SANAA NA TAALUMA NI MSINGI WA MAENDELEO YA WANAFUNZI KATIKA TAIFA" Yamejumuisha Jumla ya Washiriki 189 toka katika shule mbalimbali za Wilaya ya Chamwino.
Maafisa toka idaya ya Elimu Sekondari pamoja na baadhi ya Walimu wa Shule za Sekondari.
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KWA MWANAMICHEZO NI:-
(i) Kuwa na nidhamu ya hali ya juu.
(ii) Usafi wa mwili na kutunza mazingira.
(iii) Kuheshimu viongozi na wanamichezo wenzako.
(iv) Kushirikiana na wenzako.
(v) Kutunza vifaa vya michezo.
(vi) Kujali na kutunza muda
(vii) Kubuni mbinu mbali mbali za kushinda.
(viii) Kujituma katika mazoezi na michezo.
(ix) Kuwa mzalendo.
Picha za Pamoja za Washiriki toka katika Tarafa Tano za Wilaya ya Chamwino.
Wanamichezo Toka Tarafa ya Mpwayungu.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.