UTARATIBU WA KULIPA USHURU WA HUDUMA (SERVICE LEVY)
Halmashauri ya wilaya ya Chamwino imepewa mamlaka ya kukusanya ushuru ya Huduma kwa mujibu wa sheria ya fedha ya serikali za Mitaa Namba 9 ya mwaka 1982 na sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino (Ushuru wa huduma) ya mwaka 2004.
Kodi ya huduma inalipwa na kampuni, Shirika au biashara yoyote iliyosajiliwa ndani ya Halmashauri kwa kiwango cha asilimia sifuri nukta tatu (0.3%) ya mauzo kabla ya ongezeko la thamani.
Kwa lengo la kujiridhisha na mauzo Mkurugenzi Mtendaji anaweza kumuamuru Mlipa ushuru kwa maandishi kuwasilisha nyaraka zake za mauzo za muda husika ndani ya siku 30 baada tamko hilo kutolewa.
Mfumo wa ulipaji wa kodi ni kila baada ya mwezi au miezi mitatu kupita. Malipo hayo yafanyike kabla ya Tarehe 15 ya mwezi unaofuata mara baada ya mwezi au miezi mitatu kupita kulingana na mfumo uliochagua wewe mwenyewe.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.