Home
About Us
Departments
Information Center
Photo Events
Staff Members
Contacts

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Tovuti muhimu:

CHAMWINO DISTRICT COUNCIL.

Welcome to the Official Website of Chamwino District Council, Dodoma Region:


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Chamwino
Bw. Adrian Jovin Jungu

Ndugu msomaji

Nachukua nafasi hii kujitambulisha kwako ,mimi ni mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chamwino, Wilaya iliyopo Ikulu ndogo ya Rais, nafurahi sana kuiongoza wilaya hii ambayo ni chumvi ya maendeleo ya watu wa Chamwino na Tanzania kwa ujumla  kama lilivyo jina lake kwa lugha ya wenyeji wagogo (Chamwino), pia napenda kuwafahamisha kwamba Halmashauri ya wilaya imeamua kuanzisha tovuti yake itakayokuwa inawahabarisha wananchi wake naTaifa kwa ujumla juu ya taarifa mbalimbali za kimaendeleo, kiuchumi, kijamii na kisiasa pamoja na changamoto mbalimbali zinazoigusa Halmashauri na wananchi wake.

Aidha itatumika kama njia  nzuri ya kupata mrejesho wa utoaji wahuduma, mapendekezo, ushauri na jinsi ya kushughulikia changamomto zilizopo  kwa kutumia fursa  zilizopo ili kuboresha hudumambalimbali zitolewazo kwa wananchi wote. Naamini tovuti hii itakuwa ni njia mojawapo ya kuimalisha mawasiliano na mahusiano mazuri na wananchi kiasi kwamba itatumika kupunguza kero mbalimbali kati ya Halmashauri na wananchi.

Napenda pia kuwakumbusha wananchi wote wa Chamwino kuwa suala la maendeleo ya Chamwino ni la wanachamwino wote ,jitambue kwamba wewe ni mdau muhimu sana na mbia mkubwa wa maendeleo ya chamwino hivyo timiza wajibu wako, kama kulipa ushuru lipa kwa wakati, lipa ada za leseni  mbalimbali, kwani sehemu ya fedha hizo hurudishwa kwenu kwa shughuli za maendeleo, anza sasa kwani maendeleo huanza kwa mtu mmoja mmoja.”Mabadiliko ni mimi na wewe timiza wajibu wako”

Naomba muipokee tovuti yenu ya www.chamwinodc.go.tz iwe ni kitovu cha kukupa habari za uhakika saa 24 siku 7 za juma, asanteni sana.


NAFASI ZA UWEKEZAJI:
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino inakaribisha wawekezaji kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi, ili kukuza uchumi.

Maeneo ya uwekezaji ni pamoja na kilimo, ufugaji, viwanda, Taasisi mbalimbali, shughuli za misitu, madini na uhifadhi wa misitu.

KILIMO NA UFUGAJI
Licha ya hali ya ukame inayokabili mkoa wa Dodoma, wilaya ya Chamwino inayo hazina kubwa ya maji ya ardhini ambayo yameiwezesha wilaya kuanzisha na kuusimamia kwa mafanikio mradi wa wakulima wadogowadogo wa zabibu wa Chinangali II ambao una wakulima 300 wanaozalisha zao la zabibu.
Latest News

 

 

 

 

 

Notice Board

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Calendar

Copyright © 2014 - Chamwino DC: All rights reserved                                                                                                                                                                      Designed by: Borrybrown (0764-013922)