Maafisa kutoka Ofisi ya Rais Utumishi wakiongozwa na Ndg. Rashidi Shedafa wakishirikiana na wataalam kutoka Halmashauri wameendesha mafunzo ya mfumo wa e-utendaji kwa Wakuu wa Idara, Sehemu, Watendaji wa Kata, Wakuu wa Shule, Walimu Wakuu na Waganga Wafawidhi ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Mafunzo hayo yamefanyika leo Julai 8, 2025 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri yenye lengo la kuendelea kuwajengea uwezo watumishi ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino katika kujaza majukumu yao ya kila siku.
Mfumo wa e- utendaji umekuwa ukitumiwa na watumishi wa ngazi mbalimbali wa Serikali kujaza majukumu yao ya kila siku na kufanyiwa tathmini za utendaji wa kazi zao kupitia mfumo huo.
Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Ndg. Tito Mganwa alianza kwa kuwapongeza Watumishi kwa kazi kubwa waliyoifanya katika mwaka wa fedha uliyoisha wa 2024/2025 kwa kuiwezesha Halmashauri kufikisha wastani wa asilimia 96.7 na hivyo kuifanya Halmashauri kushika nafasi za juu ngazi ya Taifa katika mfumo wa E-Utendaji.
Pamoja na pongezi hizo Ndg. Mganwa amewataka watumishi kuongeza juhudi katika utekelezaji wa majukumu katika mfumo huo ili kuhakikisha Halmashauri inafikisha asilimia 100 kwa mwaka wa fedha mpya wa 2025/2026.
“Asilimia 96 ni nzuri tumejipongeza lakini tuwe na malengo ya kufikisha asilimia 100 na inawezekana tuwe na malengo makubwa 100 iwe ndo lengo na iwe jitihada yetu ya kila siku.”Alisema Ndg. Mganwa.
Sanjari na hilo, Mkurugenzi Mtendaji amewahasa Watendaji wa Kata kuhakikisha wanasimamia vyema ukusanyaji wa mapato ili kuzuia upotevu mkubwa wa mapato katika maeneo yao.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.