Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Khatibu Kazungu ameitaka Halmashauri ya wilaya ya Chamwino kubuni vyanzo vipya vya mapato, ikiambatana na kuandaa mpango mkakati wa kukuza uwekezaji ili kuvutia wawekezaji na hatimaye kuchochea maendelo ya mtu mmoja mmoja, Halmshauri pamoja na MKoa wa Dodoma kwa ujumla.
Dkt. Kazungu ametoa maelekezo hayo leo Septemba 18, 2025 alipofanya ziara katika Makao Makuu ya Halmashauri ya Chamwino kwa lengo la kujitambulisha kwa watumishi wa Halmashauri hiyo. Pamoja na hayo, ametaka mipango na mikakati yote inayofanywa na Halmashauri izingatie mpango wa maendelo endelevu na iendane na Dira ya Taifa ya mwaka 2050.
“Tukumbuke kwamba nchi hii inaongozwa na dira ya 2050, na katika dira ile kufikia mwaka 2050 tunatarajia kwa mfano Tanzania itakuwa ni nchi ya kwanza katika bara la Aafrika kwa uzalishaji wa chakula. Kwahiyo, kila mmoja kwa nafsi yake ana wajibu wa kuhakikisha kwamba anatekeleza majukumu yake kwa weledi, kwa juhudi, na maarifa ili kuhakikisha tunafikia malengo ya dira hiyo.”
Aidha, amewataka watumishi kufanya kazi kwa kufuata sheria, kanuni pamoja na taratibu za utumishi wa umma wakati wa kutekeleza majukumu ya kazi. Vilevile, amewasihi kujitokeza tarehe Oktoba 29, 2025 kutekeleza haki yao ya kikatiba ya kupiga kura ya kuwachagua Madiwani, Wabunge na Rais.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.