Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino ikiongozwa na Kaimu Afisa Mipango Happiness Kapinga akimuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji, leo Oktoba 03, 2025 imefanya ziara ya kukagua ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya Halmashauri, ili kuboresha huduma za kijamii kwa wananchi.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Chitabuli, Ujenzi wa Shule mpya ya Msingi Manyemba, ujenzi wa madarasa 2 mapya na matundu 8 ya vyoo katika Shule ya Sekondari Segala, ujenzi wa matundu 8 ya vyoo katika Shule ya Sekondari Manchali, na ukarabati wa miundombinu ya Shule ya Msingi Membe.
Kapinga ametoa wito kwa wasimamizi wa miradi hiyo kuisimamaia vizuri katika hatua zote za ujenzi na pale itakapoanza kutoa huduma ili iweze kudumu. Aidha, amesisitiza kukamilishwa kwa wakati kwa miradi hiyo ili ianze kutoa huduma kwa wananchi kama ilivyokusudiwa.
“Miradi hii imeletwa ili kuboresha huduma za kijamii kwa wananchi. Hivyo, ni vizuri ikamilike kwa wakati ili ihudumie wananchi kwasababu hilo ndilo lengo.”
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.