Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Ndg: Tito P. Mganwa leo Julai 15, 2025 ameendesha kikao kazi cha Watumishi wa makao makuu ya Halmashauri ya Chamwino ambacho kililenga kufanya tathimini ya utendaji kazi kwa mwaka uliopita, kuweka mikakati ya mwaka huu wa fedha wa 2025/2025 pamoja na kusikiliza changamoto mbalimbali za kiutendaji kutoka kwa watumishi. Kikao kazi hicho kimefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Chamwino.
Akifungua kikao hicho Mkurugenzi aliwapongeza watumishi kwa maeneo ambayo waliweza kufanya vizuri kwa mwaka wa fedha uliopita ambapo alisema kuna maeneo wameweza kuvuka hadi asilimia mia moja na miongoni mwa hayo ni suala la ukusanyaji wa mapato .
Naye Kaimu Afisa Mipango wa Wilaya Ndg: Gaspar Baltazar aliwasilisha hali ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka uliopita pamoja na bajeti iliyopitishwa kwa mwaka huu wa fedha kwa mapato ya ndani na kueleza kuwa watajikita kuhakikisha màpato hayo yanakusanywa kwa asilimia mia moja na kwamba mapato hayo yatakayopatikana kwa asil8mia kubwa yatakwenda kwenye miradi ya maendeleo hususani itakayowezesha Halmashauri kuongeza mapato.
Nao watumishi walijadili na kutoa maoni, ushauri na changamoto mbalimbali za kiutendaji kwa lengo la kuleta ufanisi katika kazi na kwa maendeleo ya Halmashauri nzima ya Chamwino ambapo Menejimenti ya Halmashauri ilizipatia majibu pamoja kuahidi kufanyia kazi ushauri na maoni yote mazuri yaliyotolewa na watumishi.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.