"Mifugo tuliyonayo ni mingi , ng' ombe peke yake tulionao ni ml. 35.3, kwa Afrika sisi ni wa pili kwa kuwa na ng'ombe wengi baada ya Ethiopia.Tunautajiri mwingi ambao umejificha ndani yetui ni lazima kuubadilisha ili uweze kubadilisha maisha ya Watanzaniana kuondokana na hali duni. Na ndio maana wao kama wizara ya mifugo wamekuja na mpango wa mabadiliko".
Maneno hayo yamesemwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Mashauri Ndaki alipokuwa kwenye hafla ya ugawaji wa madume bora kwa vikundi vya wafugaji iliyofanyika Wilayani Chamwino Novemba 24, 2022 katika viwanja vya Ofisi ya kilimo.
Ameeleza kuwa lengo la kufanya mabadiliko makubwa kwenye sekta ya mifugo ni kutokana na kuwa na mifugo yenye tija ndogo. Ng'ombe wanauzito kidogo na wanatoa maziwa kidogo..
"Tunafunga kiasili ufugaji ambao hausaidii sana kuchechemua uchumi wetu na uchumi wa kaya". Alisema Mhe. Waziri Mashimba.
'Masoko tuliyonayo ndani na nje hayahitaji aina ya mifugo tuliyonayo na hasa nyama. Nyama inahitajika na soko la Ulaya, China".
Alieleza kuwa wanaviwanda vya kusindika nyama lakini havina malighafi, hivyo shughuli hii ni mojawapo ya kutekeleza maboresho ya sekta ya mifugo na wameamua kufanya maboresho makubwa matatu.
Jambo la kwanza ni uhamilishaji wa koo safi na tayari wameahanunua mtambo mkubwa kwa ml. 600 walizopewa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan na uhimilishaji utafanyika nchi nzima. Na ng'ombe hao waliofanyiwa uhamilishaji watakuwa na uwezo wa kuwa na kilo 150 hadi 200 kwa ng'ombemmoja.
Jambo la pili katika maboresho ni kugawa madume bora ambayo yatasaidia kusaidia kubadilisha ng'ombe waliopo sasa. Alieleza madume wanayoyagawa ni madume ya nyama na baadae watagawa madume kwa ajili ya maziwa. Uzinduzi huu utakuwa ni kwa nchi nzima .
Aliendelea kueleza kuwa ng'ombe hawa watakuwa na uwezo wa kuzalisha maziwa kati ya lita 5 hadi 10 kwa ng'ombe mmoja. "Maziwa yatakayozalishwa kwa ng'ombe mmoja ni kati ya lita 5 hadi 10 kwa ng'ombe mmoja.
Maboresho ya tatu yaliyoelezwa ni njia ya kunenepesha mifugo na bl.4.4 zimetengwa kwa ajili ya unenepeshaji kwenye vituo atamizi ambavyo wamepewa vijana. Kwa kufanya hivyo watawatengenezea ajira vijana. Vilevile alieleza kuwa kwa kufanya hivyo pia watabadilisha akili ya wafugaji. Kupitia vijana hao wafugaji wataweza kubadili fikra zao.
Madume yaliyogawiwa kwa vikundi vya wafugaji ni 50 na kila moja linauwezo wa kupanda majike 25 na linauwezo wa wa kupanda kwa miaka minane.
Ilielezwa kuwa madume hayo wameyagawa bure kwa wafugaji lakini serikali imeyanunua kwa gharama kubwa, dume moja limenunuliwa kwa shilingi ml.2.5, hivyo aliomba watakaogawiwa wayatunze.
"Watakaogawiwa watunze madume haya, yanahitaji kuogeshwa ili yasipate kupe na hayatakiwi kuchungwa.Wanapewa bure lakini Serikali haikuyapata bure, dume moja limenunuliwa shilingi ml.2.5". Alisema Mhe. Waziri.
Aidha aliwaelekeza kuwa wasiwe wachoyo kama wanamajike machache wampe mwenye majike mengi.
Naye mwalilishi wa mbunge jimbo la Chamwino ambaye ni Katibu wake ndugu Muhsini Mulokozi pamoja na mwenyekiti wa wafugaj ndugu John Kochochoi walimshukuru Mhe. Waziri kwa madume hayo na kumuomba amfikishie shukrani zo kwa Mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassan. Aliahidi kusimamia na kuyatunza madume hayo waliyopewa.
Naye Mkuu wa wilaya ya Chamwino Mhe. Gift Isaya Msuya alishukuru kwa kupata madume hayo na kuahidi kuwa hayatauzwa na watasimamia wafugaji waweze kuyatunza na alisisitiza wafugaji wasiwe wachoyo bali waende wakawape na wengine.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.