Waziri wa Afya Mh. Jenista Mhagama ameongoza hafla ya ugawaji wa mashine 185 za upimaji wa vimelea vya kifua kikuu pamoja na kuzindua mpango harakishi wa kuibua wagonjwa wa kifua kikuu leo January 6, 2024. Hafla hiyo ilifanyika katika Kituo cha Afya Chamwino, Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino.
Mashine hizo 185 zitasambazwa katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara pamoja na mikoa miwili (2) ya Tanzania Visiwani (Zanzibar) wakati huo Halmashauri zipatazo 76 katika mikoa 9 zitahusika katika mpango harakishi wa kuibua wagonjwa wa kifua kikuu
Akizungumza katika hafla hiyo Mh. Mhagama Waziri wa Afya amesema lengo la kuzinduliwa kwa mpango harakishi wa kuibua wagonjwa wa kifua kikuu ni kuhakikisha kila Mtanzania anafikiwa ili kuwa na uhakika wa afya za Wananchi wote kwakuwa vifaa hivyo vinabebeka na kuweza kumfikia Mwananchi mahali popote.
Sanjari na hilo, Mh. Mhagama amesisitiza juu ya umuhimu wa kampeni hiyo ili kuhakikisha Nchi inafanya kazi kwa ushirikiano kati ya Serikali na Wananchi ili Watanzania wengi waweze kujitokeza kupima ugonjwa huo wa kifua kikuu unaoambukiza kwa njia ya hewa unakoma ifikapo 2030.
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mh. Janeth Mayanja ambaye pia alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary Senyamule katika hafla hiyo amemshukuru Waziri Mhagama kwa kuichagua Wilaya ya Chamwino kufanya hafla hiyo sambamba na kumhakikishia kuendelea kuwahudumia Wananchi ili kupata huduma bora
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.