Na Brian Machange-Chamwino
Waziri wa Nchi OR-Tawala Za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Ummy Mwalimu amesema serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan itamuenzi aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dr. John Pombe Joseph Magufuli kwa kumalizia ukamilishaji wa Ujenzi wa Hospitali ya Uhuru iliyopo Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Waziri Ummy ameyasema hayo leo Aprili 14, 2021 mara baada ya kukagua maendeleo katika Hospitali ya Uhuru, Wilayani Chamwino, Mkoani Dodoma.
Waziri Ummy amewatoa hofu wananchi wa Chamwino na Watanzania kwa ujumla kuwa watahakikisha wanamuenzi hayati Dkt John Pombe Magufuli kwa Kuendeleza miradi aliyoianzisha hususani Hospitali hii ya Uhuru kwakuanzisha mchakato wa Ujenzi wa majengo ya awamu ya pili yatakayojumuisha wodi za kulaza wagonjwa unaotarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.7
Kuhusu watumishi wa afya katika Hospitali hiyo, Waziri Ummy amewataka kufanyakazi kwa kujituma,kujitolea na kufuata maadili ya kazi yao wanapotoa huduma kwa wananchi na kutoa kauli nzuri kwa wagonjwa wanapowahudumia.
Aidha amewatoa hofu watumishi wanaofanyakazi za kujitolea katika Hospitali hiyo, serikali itawapa kipaumbele katika ajira zitakazotolewa huku akitoa maagizo kwa Mkurugenzi Mtendaji na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Chamwino kuandaa kanzidata ya watumishi wote wanaojitolea kwenye Hospitali hiyo.
Katika hatua nyingine, Waziri Ummy ametoa wito kwa wananchi wa Chamwino na mikoa jirani kuhakikisha wanajiunga na mfuko wa bima ya Afya ya Jamii iliwaweze kufaidi huduma zinatolewazo na Hospitali ya Uhuru.
Viongozi wa Mkoa wa Dodoma wakimkaribisha Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Mhe. Ummy Mwalimu (MB) alipotembelea Hospitali ya Uhuru Wilayani Chamwino Aprili 14, 2021
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.