Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino na watumishi waliopo makao makuu ya ya Halmashauri hiyowamekutana na kufanyà kikao cha tathimini ya utendaji kazi kwa mwaka uliopita wa 2023/2024 na kuweka alengo kwa mwaka wa fedha 2024/2025 ambao umeanza leo Julai 1, 2024.
Kikao hicho kimefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri na kimeongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chamwino Ndg: Tito P. Mganwa.
Katika kikao hicho watumishi wamejadili mafanikio na changamoto mbalimbali zilizojitokeza kwa mwaka uliopita na kuweka malengo ya kuboresha pale ambapo hawakufanya vizuri kwa mwaka huu wa fedha ulioanza.
Aidha katika kuhitimisha Mkurugenzi amesisitiza watumishi kufanya kazi kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa Umma, Ameelekeza watumishi kufanya kazi kama timu. Ameshukuru pia kwa maoni yote yaliyotolewa na kila mtumishi na ameahidi yeye na menejimenti kukutana na kuyafanyia kazi.
Mkurugenzi amesisitiza watumishi kutumia mifumo ya Serikali ikiwemo mfumo wa PEPMIS ambapo amewataka watumishi kuhakikisha wanajaza mjaukumu yao wanayoyatekeleza kila siku ikiwa ni pamoja na ruhusa na likizo.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.