Msimamizi wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa Wilaya ya Chamwino Ndg. Tito P. Mganwa amefungua mafunzo kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa leo Oktoba 4, 2024 Wilayani Chamwino.
Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi wote wa vituo 813 vya uchaguzi Wilaya ya Chamwino.
Aidha, wasimamizi wasaidizi hao wa uchaguzi wamekula viapo vya utii, uadilifu, uaminifu na kutunza siri wakati na baada ya zoezi hilo la uchaguzi.
Zoezi la uandikishaji wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za mitaa linatarajiwa kuanza tarehe 11 hadi 20 Oktoba 2024 na uchaguzi huo utafanyika tarehe 27 Novemba 2024.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.