Mafunzo kwa wasimamizi wa mikopo inayotolewa na Halmashauri kwa ngazi ya mamlaka za Serikali za mitaa yametolewa leo Oktoba 5, 2024 katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino.
Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo wasimamizi hao wa mikopo ngazi ya mamlaka za serikali za mitaa ili kuweza kusimamia vizuri vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ambao ni wanafuaika wa mikopo ya asilimia 10 kutoka Halmashauri.
Akizungumza Wakati akifungua mafunzo hayo Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Chamwino Bi. Zaina Msangi amesema mafunzo hayo yanalenga pia kufundisha kuhusu kanuni, mwongozo na mfumo mpya ulioboreshwa wa utoaji wa mikopo ikiwemo kuwepo kwa kamati za mikopo za kata, Halmasahauri na wilaya ili kuhakiki maombi ya mikopo kabla ya vikundi kupatiwa mikopo hiyo.
Aidha, Katika mafunzo hayo maafisa maendeleo ya jamii ngazi ya kata wameelekezwa kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kuunda vikundi katika maeneo yao ili kuweza kuchukua mikopo hiyo na kuanzisha miradi itakayowawezesha kujikwamua kiuchumi.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.