Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndg. Mary Chatanda amesema uwepo wa Mikopo kwa Wanawake na vijana wenye ulemavu ni fursa katika jamii na watumiaji wa mikopo hiyo kwani inaongeza mapato kwa Jamii.
Ndg.Chatanda ameyasema hayo leo tarehe 25 Novemba 2023 katika kikao cha mapokezi ya ziara yake Katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Mkoa wa Dodoma.
“Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza kwa Waziri wa TAMISEMI ili kuepusha na kupunguza changamoto za mikopo ya kausha damu na mwendokasi kwa wananchi wake.
“Wanawake na vijana wenye ulemavu wanashauriwa watumie mikopo iiliyoletwa ili kutatua changamoto zinazo wakabili na kukopeshwa kupitia mabenki na wenye vikundi viandaliwe ili waweze kupewa mafunzo ya umuhimu na faida za mikopo kwa wananchama wao” amesema Chatanda.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Gift Isaya Msuya amesema Serikali ya awamu ya Sita imeleta zaidi ya Bilion 111 kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa shule za msingi, Sekondari na ujenzi wa Vyuo vya ufundi VETA.
“Lengo la Rais kwa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino ni kuhakikisha watoto wanapata Elimu iliyobora na yenye uhakika ili waweze kutimiza Malengo Yao katika maisha Yao ya baadae” Amesema Mhe. Msuya.
Vilevile Ndg.Chatanda amefanya ziara ya kukagua miradi ya Hospitali ya Wilaya ya Chamwino yenye thamani ya Shilingi Bilioni 3.1, kukagua Mradi wa Chuo cha VETA wenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.4 na kusikiliza kero za wananchi pamoja na kuzitatua.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.