Wanawake wa Wilaya ya Chamwino waonywa dhidi ya mila, desturi na taratibu potofu za jamii zinazohusu masuala ya ulishaji watoto.Hayo yamesemwa hivi karibuni na kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri (W) ya Chamwino Bi. Sophia Swai katika Maadhimisho ya Kilele cha Wiki ya Unyonyeshaji Duniani ambapo kiwilaya yamefanyika katika Kata ya Mlowa Barabarani kwenye viwanja vya Hospitali ya Wilaya.
Bi. Sophia Swai amebainisha kuwa mojawapo ya taratibu hizo zinahusu kuwaanzishia watoto wachanga vyakula vya nyongeza mapema kabla hawajatimiza umri wa miezi sita kama wataalamu wa Afya wanavyopendekeza.
"Imethibitika kuwa unyonyeshaji wa maziwa ya mama pekee kwa watoto wachanga huimarisha kinga ya mwili nankuepusha maradhi yatokanayo na utapiamlo na upungufu wa kinga ya mwili wa watoto wachanga" alisema
Kwa upande mwingine ameipongeza Idara ya Afya pamoja na wadau wa Lishe ( Umoja wa Ulaya(EU), WFP, TAREHA, na RECODA), Maendeleo ya jamii kwa mpangilio mzuri wa Maadhimisho ya Kilele cha wiki ya Unyonyeshaji akiamini kwamba yataendelea kuadhimishwa kila mwaka kwa makusudi yakuleta mwamko katika jamii na wadau mbalimbali wa lishe juu ya harakati za kupunguza utapiamlo, vifo vya watoto wachanga na wadogo vitokanavyo na unyonyeshaji duni wa maziwa ya mama, pamoja na lishe duni ya mama na mtoto.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.