Wataalam wa Ardhi na mifugo wamefanya kikao na wanachi wa kata ya Dabalo Wilaya Chamwino kwa lengo la kutoa elimu kuhusu mradi wa kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia rasilimali za ardhi utakaotekelezwa katika vijiji vya Nayu na Manyemba.
Kikao hicho kimefanyika Agosti 2, 2023 katika kijiji cha Nayu na Manyemba ambapo wananchi wamewasilisha hoja na changamoto zinazowapa hofu katika kutekeleza mradi huo.
Akizungumza katika kikao hicho Jafari Abdallah, Afisa tarafa Itiso aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Gifty Msuya, alisema mradi huo utasaidia kuinua uchumi kwa wakina mama na jamii nzima.
Alisema wanaume wanapaswa kutoa ushurikiano kwa wake zao kuhakikisha wanapimiwa maeneo yao ili kuondoa migogoro na hofu katika familia.
“Niwaombe sana kina baba tuwaunge mkono na kushirikiana nao ili tuende tukainuke kiuchumi, lakini pia niwaombe kina mama mmepata mradi huu msikae nyuma mtoke muende mkajishughulishe mkajitoe kwenye miradi hii mnyanyuke kiuchumi na mtoke katika hali mliyo nayo sasa”.
“Kwahiyo Mhe. Mkuu wa Wilaya anawaomba sana Serikali inawapenda sana toeni ushirikiano ili kazi iende na itekelezwe bila vikwazo”, alisema.
Aidha kwa upande wake Enock Mligo, Afisa Ardhi wa Halmashauri Chamwino amewatoa hofu wanacnhi kwani maeneo yatapimwa bila gharama zozote zile na watawezeshwa katika masuala ya kilimo.
Amesisitaza kuwa hati miliki zitako tolewa zitaongeza thamani ya ardhi na kuweza kukuza uchumi wa mwanachi husika.
“Mnapimiwa maeneo yenu bure na mnawezeshwa kwenye masuala ya kilimo, Sambamba na hili hii hatimiliki itaenda kuongeza thamani ya eneo”, alisema.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.