Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Staki Senyamule leo April 20, 2024 amefanya ziara ya kikazi Wilayani Chamwino na kukagua miradi na kusikiliza kero za wananchi.
Kkuhusu kero ya ukosefu wa soko la zabibu na ombi la kuwa na bodi ya zao la zabibu ilielezwq kuwa kwa sasa Serikali inakamilisha ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza mchuzi wa zabibu ambapo kitakapokamilika kitaondoa tatizo la kuharibika kwa zabibu.
"Kumekuwa na changamoto kubwa sana ya soko la zabibu ambalo l8mekuwa likiwasumbua sana wakulima wa zabibu, jambo ambalo Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia ililiona hili. Pale kwenye shamba la Chinangali tunajenga kiwanda cha Serikali ambacho kitakuwa kinauwezo wa kuwahudumia wananchi wote walioko kwenye maeneo ya Mvumi misioni, Mvumi Makulu, Makang'wa, Handali pamoja Nghahelezi wenye zabibu nyingi." Alisema Godfrey Mnyamale.
"Kiwanda kile kipo kwenye hatua za mwisho za ujenzi, mkandarasi anatarajiwa kuingiza mitambo mwezi wa tano, tunatarajia kwa hatua za awali tunaweza kupata zabibu za kwanza za mwezi wa tisa ziingie kwenye kile kiwanda." Alisema Mnyamale
Kuhusu suala la Bodi ya zabibu mkuu wa Idara ya kilimo ameeleza suala hili linashughulikiwa na Mrajisi wa ushirika na wameanza hatua ya kwanza ya kutengeneza chama cha ushirika. Amewaomba wakulima waendelee kuiamini Serikali na tunaamini baada ya muda mfupi changamoto ya masoko ya zqbibu itakuwa imeondoka.
Akizungumza kwenye mkutano huo wa hadhara Mkuu wa mkoa alieleza kuwa kazi ya Serikali ni kuwatafutia wananchi masoko. Alimpongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan k2a kutoa kipaumbele kwa sekta binafsi kutambuliwa na kutengeneza mazingira mazuri ili kuweza kujiletea maendeleo bila vikwazo.
Kuhusu ulimaji wa zabibu niendelee kuwahimiza kwani ukombozi huo unakuja wa soko la uhakika wa kuuza mchuzi au zabibu yetu katika njia ya mchuzi na kufanya tusipate shida tena. Hiyo itakuwa ni historia kwa sababu Rais wetu ameweka kipaumbele kwenye suala la uchumi. Najua asilimia 90 ya wanaChamwino wanategemea kilimo. Tukiweza kufanya mapinduzi ya kilimo basi tutakuwa tumebadilisha uchumi wa mtu mmojammoja. Alisema Mkuu wa Mkoa.
Vilevile Mhe. Senyamule aliweza kuzungumzia kuhusu utalii wa kiutamaduni wa ngomq za asili na kuwasisitiza wananchi kuutangaza ulimwenguni na kuuenzi hususani ngoma za kigogo pamoja na nyimbo za kigogo ili wanaofanya utamaduni huu waweze kuinuka kiuchumi kupitia hizo.
Utalii mwingine aliouhimiza Mkuu wa mkoa ni utalii wa zabibu ambayo kwa Tanzania inalimwa Dodoma pekee na kwa Afrika mashariki pia.
"Watakuja watu kwenye mkulima mwenye shamba bora wamlipe pesa ili walitembelee na kuwaelezea unavyolima, unavyopanda na kuvuna. Alisisitiza wakulima walime kwa ubora ili iwe kivutio siyo tu kwa kuuza bali oia kwa utalii." Alisema Mkuu wa mkoa.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.