Afisa Elimu Msingi Wilaya ya Chamwino Bi. Zaina Kishwegwe amesema kuwa wanafunzi wilayani hapa wameonyesha dalili nzuri ya kufaulu mitihani yao ya kuhitimu darasa la saba inayotarajiwa kufanyika tarehe 11 hadi 12 septemba 2019 kufuatia ufaulu wanaoupata katka mitihani mbalimbali.
Kauli hiyo ameitoa baada ya matokeo ya mtihani wa utayari (mock) uliofanywa na wanafunzi hodari 120 kutoka kwenye shule zote za msingi za Wilaya ya Chamwino. Mtihani huo uifanyika tarehe 23 Agosti, 2019 katika shule ya msingi Buigiri Misheni na kusimamiwa na Maafisa Elimu Kata mbalimbali.
Bi. Zaina ameeleza kuwa lengo la mtihani huo nikutathmini ‘ufaulu wa juu’ katika mtihani wa darasa ili kuweka juhudi zaidi katika kipindi kilichobaki ili kufikia lengo ambalo Halmashauri imejiwekea la kuhakikisha wanafunzi wote wanafaulu elimu ya msingi na kujiunga na kidato cha kwanza.
“Aidha napenda kuwashukuru walimu, maafisa elimu wa ngazi za wilaya na kata, wazazi pamoja na wadau wote kwa kwa kazi kubwa ya kuwaandaa vijana kwani hata kwenye mtihani wa mock Mkoa, Wilaya ya Chamwino imeshika nafasi ya tatu na shule ya msingi Nyerere iliyopo tarafa ya Mvumi iliongoza kimkoa.” Alimalizia Bi Zainab Kishegwe
Wafunzi wote 120 wamepatiwa zawadi mbalimbali ikiwa ni fedha taslimu na mikebe ya kutunzia vifaa ambavyo watavitumia hata watakapojiunga na masomo yao ya sekondari.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.