Na Brian Machange - Chamwino
Wanafunzi wapatao 5056 waliofaulu mtihani wa kuhitimu Elimu ya Msingi mwaka 2020 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza 2021 toka katika shule 121 za msingi Wilayani Chamwino.
Akitoa takwimu hizo Kaimu Afisa Elimu wa shule za msingi Mwalimu Agripina Kanyabuhura, amesema kuwa wanafunzi waliofaulu mtihani wa kuhitimu Elimu ya Msingi kwa mwaka 2020 ni 5056 kati yao Wavulana 2707 na Wasichana 2351.
Mwl. Kanyabuhura ameeleza kuwa, kutokana na kuongezeka kwa ufaulu mwaka huu jumla ya wanafunzi 1963 hawakuweza kuchaguliwa kwa sababu ya upungufu wa vyumba takribani 43 vya madarasa kwa shule za sekondari katika Halmashauri, hata hivyo juhudi zinafanyika kuhakikisha vyumba hivyo vinajengwa na wanafunzi wote waliofaulu wanajiunga na kidato cha kwanza ifikapo Januari 2021.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino ina jumla ya shule za msingi 121 zikiwemo shule 119 zinazomilikiwa na serikali na shule 2 zinazomilikiwa na taasisi binafsi. Kwa mwaka 2020 idadi ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kuhitimu Elimu ya msingi walikuwa jumla 7021 miongoni mwao wakiwemo wavulana 3511 na wasichana 3510.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.