Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Staki Senyamule Julai 23, 2024 amefanya ziara ya kikazi Kata ya Fufu wilayani Chamwino kwa lengo la kugawa hati miliki za kimila pamoja na kusikiliza kero za wananchi.
Akizungumza kabla ya kukabidhi hati hizo Mkuu wa mkoa amesema mara nyingi kumekuwa na migogoro ya wakulima na wafugaji.
" Mara nyingi wafugaji wamesema tumenyang'anywa ardhi yetu, tukajiuliza unaposema ya kwako unamaanisha nini, wanasema ninafuga hapa miaka mingi baba yangu nimemkuta anafuga hapa lakini ukimuuliza umiliki wake hana kitu chochote kinachoonesha umiliki. Kwa maana hiyo akija mtu mwingine mwenye uthibitisho wa umiliki wa eneo anaendelea kulimiliki kwa kuwa yeye hana karatasi ya umiliki."
" Ardhi inamilikiwa kisheria na kisheria ni kuwa na karatasi inayoitwa hati. Wakulima walianza kuchangamka mapema kidogo kuliko wafugaji na ilikuwa kazi kubwa kuwaelimisha wafugaji kuwa na wao wanapaswa kumiliki ardhi kisheria ili watambulike." Alisema Senyamule.
Aidha mkuu wa mkoa alieleza, " Nidhamira ya Mhe. Rais wakulima wakae kwa utulivu na wamiliki ardhi kama haki yao ya msingi, lakini alijua kwa kufanya hivyo itapunguza au itaondoa migogiro kwa kiasi kikubwa migogoro ya wakukima na wafugaji, lakini pia alijua katika mkoa wa Dodoma ipo migogoro ya kihistoria ambayo haiishi kila mwaka kutokana na changamoto hizo za umiliki na hivyo kuwa na migogoro isiyofika mwisho." Alisema senyamule.
Alimpongeza ndugu Lubeleja Katibu wa wafugaji wilayani chamwino na wenzake kwa kufanya wafugaji wakajua umuhimu wa kutoa gharama pamoja na viongozi wengine wote kutoka Kamishina wa ardhi pamoja na viongozi ngazi ya Wilaya kwa ushiriki wao katika zoezi hilo.
"Nafahamu kumekuwa na migogoro ya ardhi ya muda mrefu Mkoa wa wa Dodoma ambapo huwezi kuacha kutaja Izava, huwezi kuacha kutaja Fufu, mara nyingine tumeitisha vikao vya mkoa mzima na kuulizana tunafanyaje kuhusu Fufu, tunafanyaje kuhusu Izava kwa sababu ilifikia hatua kumesababishwa vifo, kumesababishwa ulemavu, maumivu kwa sababu watu wamepigwa kwa kugombania maeneo ya malisho. Alisema Mkuu wa Mkoa.
Vilevile Mkuu wa Mkoa ameeleza furaha yake kwa kumalizika kwa mgogoro wa mipaka wa Izava na Kongwa.
Aidha alieleza kuwa hati ni karatasi lakini dhamira ya kutoleta migogoro ipo kwenye kichwa cha binadamu, hati hii itakusaidia akiingia mwenzako na kuanza kulima utasema amekuingilia kwa kuwa utakuwa na karatasi inayoonyesha kuwa eneo ni lako na ndipo atakuja kiongozi na kusema eno ni la kwako. Aliongeza kusema kuwa wanataka kila mmoja afurahie kuishi mkoa wa Dodoma.
Mkuu wa mkoa pia alieleza kuwa widhara ya kilimo inayo fursa ya kuwajengea visima na kuwapatia mbegu bora za kisasa. Ameeleza kuwa kwa kufuga kisasa watweza kujiletea maendeleo. Alitolea mfano nyumba za kisasa wanazoziona na kuzitamani hata wao wataweza kuzijenga.
Naye afisa Ardhi wa Wilaya ya Chamwino Enock Mligo alieleza faida za kuwa na hati hizo za kimila ambapo zitawawezesha kupata mikopo kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo kama kuchimba visima, kujenga majosho ya kisasa, kupanda malisho pamoja na kuhifadhi mazingira kutokana na kuondokana na ufugaji holela.
Jumla ya hati ishirini za kimila zimetolewa kwa wafugaji kutoka maeneo mbalimbali ya Tarafa ya Makang'wa na jumla ya hekari 6639.19 zimeweza kupimwa kwa tarafa ya Makang'wa na Itiso.
Wananchi pia waliwasilisha kero zao na wataalam kuzipatia majibu. Aidha pia mkuu wa mkoa alitoa maelekezo kwa wataalam ili kushughulikia kero hizo.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.