Waheshimiwa Madiwani Chamwino Waombwa kugawana Rasilimali za Ujenzi
Waheshimiwa Madiwani ambao vijiji vyao vinamiradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa fedha za mpango wa Maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO - 19 wameombwa kugawana rasilimali za ujenzi na vijiji ambavyo havina rasilimali hizo.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kwemye kikao cha Baraza la Madiwani cha Robo ya kwanza kilichofanyika kwenye ukumbi wa Serikali ya kijiji cha Chamwino kwa siku mbili tarehe 28 - 29 Oktoba, 2021.
Alieleza kuwa kuna vijiji vinatekeleza miradi hiyo lakini havina rasilimali za ujenzi na hivyo kutegemea kutoka vijiji jirani.
" Kuna baadhi ya vijiji vitatekeleza miradi ya ujenzi wa madarsa lakini havina rasilimali za ujenzi hivyo naomba washirikiane katika upatikanaji wa rasilimali ili ujenzi usisuwesuwe."
Vilevile amewaomba Wah. Madiwani wawahamasishe wananchi kupatà chanjo ya UVIKO - 19 ili kujikinga na maambukizi. Aidha alieleza kuwa kwa awamu ya kwanza ya chanjo walifanikiwa kuchanja kwa asilimia mia moja ya chanjo walizogawiwa.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.