Balozi wa zao la pamba nchini Agrey Mwanri ametoa elimu kuhusu kilimo cha zao hilo kwa Wahe. Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chanwino.
Maelekezo hayo ameyatoa leo, Septemba 07, 2022 kwenye kikao maalum cha Baraza la Madiwani la mwaka kilichofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri
Akizungumza kwenye kikao hicho Mwanri amesema Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino imepangiwa kuvuna kilo milioni nne za pamba.
Aliendelea kueleza kuwa makubaliano yaliyowekwa ni walau kila Halmashauri izalishe mara mbili ya lengo walilopewa.
Mwanri alieleza kuwa Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa wameelekezwa na Mhe. Rais kuhakikisha malengo yaliyowekwa yanafikiwa.
Maelekezo ya namna ya kulima zao hilo la pamba kwa mavuno yenye tija yalitolewa ambapo kipimo ni sentimita 50 kwa 30 ambapo ukipanda kwa kipimo hiki unapata miche 4444 kwa ekari moja.
Balozi wa zao la pamba aliwahimiza wahe. Madiwani wawahimize wananchi kulima pamba kwani kupitia kilimo hicho Halmashauri itanufaika kwa kuongeza mapato pamoja na kukuza uchumi wa mwananchi mmojammoja na Halmashauri kwa ujumla.
Mkilima pamba Halmashauri itapata ushuru(produce cess) na hali ya maisha ya wananchi itakuwa nzuri." Alisema balozi wa pamba.
Aidha alieleza kuwa kwa wakulima watakaolima pamba wataletewa mbegu, viuatilifu na mifuko vitavyotolewa kwa mkopo na ambao utalipwa baada ya kuvuna na kuuza.
" Tutaleta mbegu, viuatilifu na mifuko vitakavyokopeshwa na mkulima ataulipa mkopo huo baada ya kuvuna na kuuza pamba yake." Alisema balozi wa pamba.
Alihimiza watumie fursa hiyo ambayo imetolewa na Serikali kwani kilimo cha pamba ulimaji wake hauhitaji mvua nyingi na kwa hali ya hewa ya Chamwino zao linaweza kustawi vizuri.
' Fursa hazitolewi, fursa zinachukuliwa, hivyo tumieni fursa hii iliyotolewa na Serikali kwani zao la pamba halihitaji mvua za kitimutimu kama zak la mpunga au miwa." Alisema balozi wa pamba.
Vilevile alitoa maelekezo ya mambo ya kuźingatia kwenye kupanda, kupalilia, kupuliza dawa, kuvuna pamoja na vifaa vinavyofaa kwa kuvunia kwa mavuno yenye tija. Pia alieleza kwa sasa bei ya pamba kwa kilo imepanda inauzwa kwa wastani wa shilingi 2200.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.