Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Dkt.Semistatus H. Mashimba, amewataka wafugaji kushiriki katika zoezi la upimaji wa maeneo yao ili kuondokana na migogoro inayojitokeza katika jamii.
Akizungumza katika mkutano na wafugaji wa Wilaya ya Chamwino Oktoba 19, 2022, amesema lengo la zoezi hilo ni kusaidia kuondoa migogoro kati ya wafugaji na wafugaji, wakulima na wafugaji katika maeneo yao.
Amesema zoezi hilo linatarajiwa kutekelezwa kwa siku 20 na linakusudiwa kuanza tarehe 24 Mwezi huu.
“zoezi hili litaanza mapema iwezekanavyo na natarajia ndani ya siku 20 liwelimekamilika na zoezi hili rasmi litaanza tarehe ishirini na kukamilika kwa siku hizo”.
“Naomba kupata ushirikiano kutoka kwenu ili tuweze kutekeleza jambo hili kwa haraka zaidi, na jambo hili litasaidia kuondoa migogoro katika mazingira yetu tunayo ya ishi kama vile migogoro kati ya wafugaji na wafugaji pia wafugaji na wakulima,” amesema Dkt. Mashimba.
Vilevile amewaelekeza wafugaji kuwa wanapaswa kutunza nyaraka walizo nazo ili kupata taarifa za uhakika wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo.
Amesema Serikali inatengeneza miongozo mizuri kupitia zoezi hilo ili kutekeleza miradi ya josho kwaajili ya mifugo.
Aidha amewaasa wafugaji hao kuchangia gharama za upimaji wa maeneo yao.
Kwa upande wa Wafuagji wamesema wapo tayari kutoa ushirikiano ili kuepusha migogoro na kuweza kutambua mipaka yao.
Wamesema kila mfugaji alijinunulia eneo kwa ajili ya shughuli za ufugaji na zoezi hilo likikamilika litakuwa mfano kwa Wilaya zote za nchi ya Tanzania.
“Haya maeneo ni ya kwetu tunaomba tukapimiwe kwa haraka na jambo hili la upimaji litasaidia kuondokana na changamoto za kuingiliana katika mipaka yetu”.
“Pia zoezi hili likikamilika litakuwa mfano wa kuigwa kwa Halmashauri zote za nchi yetu ya Tanzania”, wamesema.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.