Serikali inawajibu wa kuweka mazingira mazuri kwa wafanyabiashara na wafanyabiashara wanawajibu wa kulipa kodi ya Serikali.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Chamwino Mhe. Gift Isaya Msuya kwenye mkutano wa Baraza la Biashara la Wilaya uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri, Novemba 27, 2023.
'Kuna suala linaitwa haki na kunasuala linaitwa wajibu, serikali inahaki ya kuwatengenezea wafanyabiashara na wawekezaji mazingira mazuri ya kufanya biashara na kuwekeza lakini upande wa pili wafanyabiashara na wawekezaji pia wanawajibu wa kuhakikisha wanalipa kodi, wanalipa tozo, wanashirikiana na Serikali kwenye masuala ya uwekezaji na kurudisha kwa jamii kama sehemu ya faida wanayoitengeneza." Alisema Mhe. Gift.
Amewaomba upande wa sekta binafsi kulisimamia na kushirikiana na Serikali bila shuruti kwa wakati mwingine hata kulipa kodi au kukata leseni mpaka washurutishwe ndipo atekeleze.
Aliwakaribisha kuwekeza kwenye miradi mikubwa inayotekelezwa ndani ya Wilaya na kutumia fursa zilizopo, alitolea mfano kuwa watu wanatoka mbali kama vile kigoma kutafuta fursa hizo.
Alieleza kuwa kwenye bwawa la Membe watashirikiana na Wizara ya mifugo kuhakikisha wanawekeza kwenye ufugaji wa samaki, na bwawa lina zaidi ya lita bilioni sita za maji yatakyokusanywa.
Adha alieleza kuwa bwawa la Membe limejengwa kimkakati na mkakati wa kwanza ni kupunguza wingi wa maji kutoka kwenye safu za milima za Wilaya ya chamwino na maeneo mengine yanayoharibu miundombinu ya barabara, madaraja. Anatamani Chamwino iwe ni mfano wa kila kitu ikiwemo utunzaji wa mazingira, upangaji wa miji na ukusanyaji wa mapato kwa kuwa ni wilaya inayobeba heshima ya Taifa letu.
Naye Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Semistatus H. Mashimba alisisitiza kuhusu suala la ushirikiano kati ya wafanyabiashara, wawekezaji na Halmashauri kwenye maeneo yote.
Naye Afisa biashara wa Wilaya Bibi Bertha Msaki alitumia mkutano huo kuelezea fursa zilizopo ndani ya Wilaya ya Chamwino ikiwemo uwekezaji kwenye kilimo na uwepo wa viwanda vidogo na vya kati.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.