Halmashauri ya Chamwino imefanya mkutano wa wadau kujadili mpango wa matumizi ya ardhi ya Wilaya ya Chamwino leo Julai 14, 2023. Mpango huu umeratibiwa chini ya mradi wa uwezeshaji wa usalama wa milki za ardhi unaoendeshwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Dunia.
Mkutano umefanyika kwenye ukumbi wamikutano wa Halmashauri na Mgeni Rasmi wa mkutano huu alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Gifty Isaya Msuya.
Katika mkutano huo maoni mbalimbali yametolewa na wadau kwa ajili ya kuuboresha na baadhi yalitolewa ufafanuzi ndani ya kikao na mengine yalichukuliwa kama maazimio kwa ajili ya kwenda kuboresha mpango huo.
Wadau mbalimbali wameshiriki kwenye kutano huu wakiwemo viongozi wa chama cha Mapinduzi na ACT Wazalendo, Wizara ya Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, Wizara ya Maliasili na Utalii, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Taasis nyingine za Serikali kama vile Mamlaka ya hali ya hewa, TAWA, Wahe. Madiwani, viongozi wa dini, Taasis binafsi, Kamati ya Ulinzi na usalama ya wilaya,Baadhi ya Wenyeviti wa Serikali za vijiji, Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata, Wakuu wa Idara za Halmashauri na watumishi mbalimbali wa Serikali.
Aidha viongozi na wadau wamempongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha mradi huu kutekelezwa Wilayani Chamwino na kwenye wilaya nyingine zinazotekeleza mradi kama huu, kwani utawezesha kuwa na maeneo yaliyopangwa vizuri na hivyo kuharakisha maendeleo na kuondoa migogoro ya ardhi.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.