Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino imefanya kikao cha wadau wa elimu Wilaya leo Februari 16, 2023, kwa lengo la kufanya tathimini kuona walichopanga na wapi walipofika katika utekelezaji wa malengo waliyojiwekea. Kikao kimefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashàuri.
Akizungumza alipokuwa akifungua kikao hicho Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Chamwino ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mheshimiwa Remidius Mwema Emmanuel amesema kama Wilaya waangalie mambo yaliyowavuta nyuma ili wayarekebishe.
Aidha Mkuu wa Wilaya alieleza kuwa Chamwino imedhamiria kuleta mapinduzi makubwa kwenye eliju kwa kuona mabadiliko kwa kila mwaka.
Katika kikao hicho Maafisa Elimu Msingi na Sekondari waliwasilisha taarifa za hali ya Elimu kila mmoja na baada hapo wajumbe walijadili nakuweka maadhimio mbalimbali yatakayoweza kusaidia katika suala la kuboresha hali ya elimu ndani ya Wilaya.
Miongoni mwa madhimio yaliyofikiwa ni pamoja na utoaji wa motisha kwa walimu kuanzia ngazi ya kijiji hadi Wilaya pamoja na maslahi na stahiki za walimu kutolewa kwa wakati.
Kila shule kulima mashamba na kuweka vitega uchumi kwa ajili ya kutoa chakula shuleni.
Walimu wakuu na Wakuu wa shule kupimwa kwa ufaulu shuleni na kutoa bendera nyeusi kwa shule zinazofanya vibaya.
Kutoa Elimu kwa wazazi, wanafunzi na jamii nzima kuhusu umuhimu wa elimu
Ufanyaji wa mazoezi na mitihani ya mara kwa mara kwa wanafunzi pamoja na kuwepo na jitihada za kuondoa alama Dna E
Suala la michezo mashuleni kupewa kipaumbele likiwemo suala la mchakamchaka
Kusimamia nidhamu za wanafunzi ikiwemo suala la viongozi wa dini kufundisha vipindi vya dini mashuleni ili kuondoa mmomonyoko wa maadili.
Kuweka makambi kwa madarasa ya Mitihani likiwemo suala la usimamizi mzuri wa prepo
Katika kikao hicho zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslim na vyeti vilitolewa kama motisha kwa shule zilizofanya vizuri kwà vigezo mbalimbali vya kielimu kwa elimu ya Msingi na Sekondari.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.