Mwaka 1991, wakuu wa nchi wanachama wa umoja wa Afrika OAU walianzisha siku ya mtoto wa Afrika kama kumbukumbu ya uasi dhidi ya wnafunzi Juni 16, 1976 huko Soweto Afrika Kusini. Wakati huo, wnafunzi watoto wadogo waliandamana, kwanza kupinga aina ya elimu duni ya kibaguzi iliyotolewa na serikali ya makaburu. Pili waliitaka serikali ya makaburu iwape ruksa kufundishwa kwa lugha zao asili. Katika maandamano hayo serikali ilitumia nguvu kuwatawanya watoto waliokuwa wakiandamana na kupelekea vifo vya watoto Zaidi ya elfu mbili.
Halmashauri ya wilaya Chamwino imeazimisha imefanya maadhimisho ya kiwilaya jumamosi ya tarehe 15, Juni 2019 kwenye viwanja vya shule ya msingi Buigiri Blind. Maadhimisho hayo yaliwaleta pamoja watoto kutoka maeneo mbalimbali na kuto fursa kwao kueleza changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo katika malezi ngazi ya familia na jamii wanazotoka.
Miongoni mwa changamoto kubwa inayoikabili jamii ya Chamwino ni pamoja na ndoa za utotoni. Hapo mchungaji wa kanisa la Agape-Kawawa alitoa ushuhuda alivyosaidia kuzuia ndoa ya mtoto mwenye umri mdogo na ukinzani na vitisho alivyovipata kutoka katika familia iliyotaka kumuozesha mtoto.
Bw. Lucas Manyala mgeni rasmi aliyemwakilishi wa mkuu wa wilaya ameitaka jamii ya Chamwino kuhakikisha watoto wanapata haki zao za msingi na mahitaji ya msingi ikiwa ni pamoja na mahitaji yao ya msingi. Pia amewataka kutafakari kauli mbiu ya mwaka huu; “Mtoto ni Msingi wa Taifa Endelevu: Tumtunze, Tumlinde na Tumuendeleze.” Bw Manyala amesema kuwa kauli mbiu hii inaweka msingi mkuu kwa ustawi wa mtoto.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Buigiri ndugu Kenneth Yindi akishirikiana na ofisi ya mkuu wa wilaya wameahidi kununua baiskeli kwa binti anayepata adha ya kusafiri umbali mrefu kwenda shuleni.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashari ya wilaya ya Chamwino Bw. Godfrey Nyamale amesema kuwa halmashauri haipo tayari kuona unyanyasaji wa watoto ukiendelea na amewashukuru wadau wa haki za watoto Bi. Rose Zakayo wa KATUKA Paralegal Organization na Bw. Petro Nziku wa Kituo cha Amani, Haki na Msaada wa Sheria kwa kuendelea kushirikiana na Halmashauri ya Chamwino.
Nao wadau wa Haki za watoto wamefungua milango zaidi kwa watoto wa Chamwino kutoa taarifa kwao wakati wote wanapokumbana na unyasaji na kuwataka watoto wajiamini kwani sharia zipo na zitawalinda.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.