Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino imetoa mikopo yenye thamani ya Tshs. 203,300,000/= kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu vilivyokidhi masharti ya kupatiwa mikopo ya Serikali.
Vikundi vilivyopewa mkopo vinajishughulisha na shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo cha bustani kwa njia za umwagiliaji, ufugqji na unenepeshaji wa mifugo, usindikajiwa mafuta, biashara ya saluni, utengenezaji wa samani na mama lishe, biashara ya kubeba mizigo na abiria yaani BODABODA na Usafi wa mazingira.
Hafla ya utoaji wa mikopo imefanyika leo Disemba 05, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ambapo mgeni Rasmi alikuwa ni Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Edson Sweti ambapo amekabidhi hundi yenye thamani ya Tshs 203,300,000/=
Akizungumza kwenye hafla hiyo Mhe. Edson Sweti amewataka wanufaika wa mikopo hiyo matumizi kuzingatia malengo waliyoombea mikopo kwani kimyume na hivyo watashindwa kutimiza malengo ya mikopo pamoja na kushindwa kurejesha marejesho.
"Hakuna mtu yeyote duniani aliyendelea pasipo kukopa' hata mimi ninamkopo benki, isipokuwa mnachotakiwa kuzingatia ni kutumia fedha mliyopewa kwa malengo yaliyokusudiwa. Isije vijana mkachukua mkopo kwenda kuolea aukina mama mkadanganywa na waume zenu kachukua kidogo kwenda kufanyia matumizi au mkaona gauni mpya ukasema utoe hapo ununue hata ndugu yako akikuomba usimpe maana utashindwa kurejesha na utakayedaiwa ni wewe uliyechukuwa mkopo." Alisema Mhe. Sweti.
Naye mwakilishi wa Mkurugenzi mtendaji Bibi Zaina Msangi ameeleza kuwa Halmashauri itaendelea kutoa mikopo kwa vikundi kila robo mwaka kulingana na upatikanaji wa fedha za mapato ya ndani. Aidha alieleza kuwa kwa mwaka huu wa fedha imetengwa bajeti ya Tshs. 243,000,000/= kwa ajili ya vikundi vya wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu.
Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji aliendelea kueleza kuwa Halmashauri inaendelea na uratibu wa utambuzi na usajili wa wafanyabiashara ndogondogo ( Machinga) ambapo mpaka sasa wafanyabiashara ndogondogo 137 wamesajiliwa na Halmashauri imepokea vitambulisho vya awali 117 vya wafanyabiashara hao toka ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya kuwakabidhi kwa ajili ya mchakato wa kupata huduma nyingine.
Vitambulisho hivyo 117 pia vimekabidhiwa kwa wajasiliamali hao wadogo
Aidha wataalam mbalimbali wamewapatia elimu vikundi na wajasiliamali wadogo wa namna ya kuendesha shughuli zao kwa tija kuwezesha kurejesha mikopo hiyo waliyopewa
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.