Naibu kamishina wa jeshi la Magereza Tanzania Bertha J. Minde amekabidhi msaada wa madawati hamsini na tano, viti thelasini na sita na meza thelasini na sita kwa niaba yaKamishina wa Magereza Tanzania katika shule ya msingi Chinangali II wilayani Chamwino.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano hayo kamishina Minde amesema anaungana na uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Chamwino na shule ya Chinangali II kumshukuru Kamishina wa Magereza kwa kutekeleza ahadi aliyotoa Septemba 2, 2023 kwenye mahafali ya darasa la saba ambapo kamishina mstaafu wa magereza kwa sasa mzee Ramadhani Nyamka aliyewakilishwa na naibu Kamishina Athumani Ambayukite.
Aliendelea kueleza kuwa katika risala yake mkuu wa shule pamoja na mafanikio alieleza changamoto ya upungufu wa thamani za ofisi pamoja na madawati hamsini na tatu. Kwa kuzingatia upatikanaji wa elimu bora jeshi la magereza limetengeneza thamani hizo zenye thamani ya Tshs. 20,825,000/= kwa ajili ya kutatua changamoto hiyo.
Naye mgeni rasmi bibi Tulinagwe Ngonile akimuakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chamwino ameshukuru kwa msaada wa vifaa hivyo na kusisitiza matunzo kwa ajili ya vifaa hivyo.
"Shule na jamii inayozunguka shule inapaswa kuhakikisha viti hivi na madawati haya vinatunzwa, siyo baada ya mwezi mmoja tunakuta dawati linaning'inia mbao au dawati limewekwa stoo limeharibika. Tuhakikishe yanatunzwa kwa kuwa na matumizi sahihi na siyo tu kuyatunza pia yalindwe. Tusije tukasikia yamepotea au yameibiwa. Azima tutunze nguvu ambayo wenzetu wa magereza wamejitoa kuhahikiSha wanalekebisha mazingira ya shule." Alisema Tulinagwe.
'
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.