Wanafunzi wa shule ya maalum ya Buigiri blind wamepokea misaada mbalimbali ya mahitaji shule kutoka kwa taasisi ya THE TUNU PINDA FOUNDATION na THE CHINA TANZANIA WOMEN EMPOWERMENT Juni 13,2024 ikiwa kama sehemu ya maadhimisho ya Siku ya mtoto wa Afrika ambayo huadhimishwa Juni 16 ya kila mwaka.
Zawadi zilizotolewa na Taasisi hizi ni pamoja na mabegi ya shule, sare za shule kwa wanafunzi wa kike na kiume na karatasi maalum za wasioona ambavyo vimegharimu jumla ya shilingi milioni kumi na tatu na laki nane.
Akizungumza kwenye hafla hiyo Mhe. Mkuu wa Wilaya Janeth Mayanja amewashukuru kwa tendo lao la huruma walilolifanya ambalo kwalo limeonyesha upendo mkubwa kwani shule zenye uhitaji kama huo zipo nyingi lakini wakaamua kuja shule maalum ya Buigiri.
Mkuu wa Wilaya pia ameshukuru kwa elimu waliyotoa kuhusu majuzi ya mtoto kwani itakuwa imewajenga wazazi na watoto pia.
Naye mama Tunu Pinda pamoja na washirika wake kutoka taasisi ya THE CHINA TANZANIA WOMEN EMPOWERMENT wamewapongeza watoto kwa risala yao nzuri na wameahidi kuyafanyia kazi changamoto zilizowasilishwa kwao.
Naye mwanafunzi Lista Mtwange akiwawakilisha wanafunzi mwenzake amewashukuru wageni hao kwa moyo wao wa upendo na kuacha watu wengine na kuona kituo chao kuwa cha muhimu sana.
Kaulimbiu ya Mtoto wa Afrika mwaka huu inasema "Elimu jumuishi kwa watoto izingatie maarifa,, maadili na stadi za kazi".
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.